Nimesikia katika gazeti moja la Kiswahili la kila siku ya kwamba, DC amepewa ripoti yenye majina ya wauzaji wa magogo na nguzo za umeme kinyume na sheria kutoka katika msitu..
Nakumbuka miaka kadhaa iliyopita, Mh. Raisi alipewa ripoti yenye majina ya Watanzania 11 vinara wa uuza wa unga (madawa ya kulevya). Tangu wakati Mh. apewe ripoti na majina hayo kumekuwa na maswali yasiyo na majibu juu ya nini wahalifu hao walichofanyiwa kwani madawa ya kulevya yamezidi kuongezeka hata kutishia ustawi wa nguvu kazi ya Taifa.
Samahanini kwa kukosa vyanzo halisi vya habari, ikiwa kama kuna mdau mwenye vyanzo halisi vya habari atoe. Nawaomba tujadili hoja JE NI SAHIHI KWA VIONGOZI WA SERIKALI KUPEWA MAJINA YA WAHALIFU BADALA YA MAJINA HAYO KUPELEKWA MAHAKAMANI? Kumbuka moja ya nguzo za demokrasia ni mgawanyo wa madaraka kati ya Mahakama, Bunge na Serikali. Karibuni wote!