Je, ni sahihi mwanaume kwenda kukaa ukweni?

Hii tabia niliikuta huku dar kwa wavulana aisee khaa mwanaume unaanza je kukaa ukweni?
Utaomba unyumba utadhubutu kukolea na kuguna?


Nitoke mie ni yule mwanaume aliyeolewa kwa kuanza kutolewa mahari, kuhamia kwa mwanamke na dhehebu kabadili toka RC to Lutheran mbaya zaidi kazi zote za kiume na kuiendeleza familia anafanya mwanamke wakati yeye ni Real Mario haaa
 
Duh, mimi nakaa mtaa jirani na wakwe ila naona sio sawa kabisa., sasa kukaa kabisa ukweni hapana asee hata kama umefulia namna gani. Bora uongee na wife arudi kwao kwa muda wewe hata kwa masela ukapotezee muda wakati unajipanga.
Zereu sana aseeee
 
Wavulana wanaweza,
Ila mwanaume wa kweli kukaa ukweni hapana.
Achilia mbali nyumbani kwao tu,na hasa ukiwa na familia
 
Kwa mimi niliyelelewa kijijini huko ndani ndani kabisa, hilo unalouliza haliwezekani, ukweni ni sehemu inayoheshimika sio mchezo, ukienda ukweni unaenda kwa shida maalumu, kama ni kusalimia ni kwa siku maalumu sio kila siku.

Aisee kabila langu lina mambo sio mchezo, huwezi kumsalimia mama mkwe kwa kushikana nae mkono.

Yaani masharti ni magumu mnooo japo nayaona yana maana ya kuweka distance ya kudumisha heshima baina na mtu na wakwe zake.

Maajabu nayaona mjini Dsm ukweni wengi wetu tunachukulia poa tu, any time mtu anapita anakula, anakunywa anasepa, wengine wanahamia kabisa ukweni.
Utasikia aisee baba mkwe kanipa chumba pale nikae maana saivi mambo yangu magumu kidogo
Kudadeki sisi kwetu hakuna hiyo, kama mambo yako magumu tafuta kwingine sio ukweni maana hata mkeo na shemeji zako watakushusha heshima
 
Marufuku kukaa ukweni.............umeanza lini tabia hiyo.....?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…