Je, ni sahihi wabunge kuapa wakiwa wameshika kitabu cha dini tofauti na dini ya Spika?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Hili swali nalielekeza Duniani kote ambako Utaratibu wa kuapisha Wabunge kwa kutumia Vitabu Vitakatifu Vya Mitume wa Mungu wa Mbinguni unatumika.

Kwa upande wa Rais haina shida kwa sababu wanakuwepo Jaji Mkuu na Mufti au Askofu.

Niko pale nasubiri Elimu.

Mungu wa Mbinguni awabariki.πŸ˜€
 
Speaker ni chombo kama ilivyo silaha au kisu, huwa hatuangalii nyama imechinjwa na kisu gani kilichotengenezwa na nani au kumilikiwa na nani
 
Nafasi ya speaker sio ya kidini, ni muwakilishi wa bunge. Anaapa mbele ya bunge si sheikh wala mchungaji
 
Haapi kwa spika wa Bunge. Anaapa kwa nafsi yake na Mungu wake kwa imani yake, wale ni mashahidi wa kiapo chake na spika ni shahidi mkuu

Ndio manayake hivyo kiapo ni imani wanaapa kwa Mungu
 
Ukisikia mtu anasema kuwa yeye ni mfanyakazi wa serikali ujue either ni mwalimu, polisi au suma-jkt
 
Wanaapa kwa dini zao sababu wanawajibika kwa Mungu kwanza kabla ya kwa serikali.
Anaeogopewa ni Mungu kwanza kabla ya serikali.
 
Kwa nini wateuliwa wasiape kwa kushika bendera ya Taifa na Jaji na Rais wakae pembeni kama mashuhuda tu?
Kuapa kwa kushika Biblia au Quran ni unafiki tu. Au kuapa mbele ya Rais ambaye pia ni mtumishi wa Serikali... Wapi na wapi? 😳
 
Daaah spika ni mungu?
Uchawa umezidi kwakweli.



KAZI ni kipimo cha UTU
 
Dini ya spika ndio kitu gani? Mambo mengine ni upumbavu hata kujadili.
 
Wabunge wenyewe kwanza nao ni mafisadi na majizi tu kama majizi mengine, hata kuapa kwa kutumia vitabu vitakatifu vya dini zao ni kuvinajisi tu hivyo vitabu. Wanamdhihaki Mungu, siku ya mwisho watachomwa motoni.
Ni afadhali wangeapa kwa kutumia katiba ya nchi tu.
 
Viapo vinashababisha hatuendelei
 
Sahihi Kabisa πŸ˜‚
 
Kwa nini wateuliwa wasiape kwa kushika bendera ya Taifa na Jaji na Rais wakae pembeni kama mashuhuda tu?
Kuapa kwa kushika Biblia au Quran ni unafiki tu. Au kuapa mbele ya Rais ambaye pia ni mtumishi wa Serikali... Wapi na wapi? 😳
Kiapo (Oath) ni Tamko au Ahadi kwamba hicho unachotamka ndicho utakachofanya au kutekeleza na Utawajibika endapo utafanya kinyume.
Kwa mantiki hiyo anayetamkiwa (anayeahidiwa) ni sharti awe anaweza kusikia au awe ni Nafsi Hai. Bendera sio Nafasi hai wala haiwezi kusikia hiloTamko au hiyo Ahadi inayotolewa. (I stand to be corrected).
 
Kwa kiasi fulani uko sahihi kulingana na mfumo uliowekwa, ambao tunapaswa kuuhoji. Tatizo la matumizi mabaya ya mamlaka kuchomoza zaidi kwenye hizi tawala zetu za kiafrika. Mamlaka hulevya na kufikia kutukuzwa mfano wa kuwa Mungumtu.
Bungeni kuna utaratibu wa kutunza kila neno linalotamkwa.... Hansard ndio neno linalotumika kuelezea utaratibu huo, kwa nini isiwe hivyo hata Serikalini?
 
Ni kweli ila sasa inakuja wanaopitisha Taratibu hizo ndo hao hao wanaotaka ziwanufaishe.
Nimekuelewa vizuri - asante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…