Je, ni sahihi Wachungaji kututafsiria Injili Wakati sisi Wenyewe tunajua Kusoma na Kuelewa?

Je, ni sahihi Wachungaji kututafsiria Injili Wakati sisi Wenyewe tunajua Kusoma na Kuelewa?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Imekuwa ni kawaida Wachungaji kutafsiri Neno la Mungu ( Injili) Wakati wa mahuburi

Lakini Biblia imeandikwa kwa Lugha inayoeleweka

Mfano Yesu baada ya kutembezwa umbali mrefu na baadaye kusulubiwa msalabani alisema " naona Kiu"

Sasa hii kauli ya " naona Kiu" imekuwa na tafsiri nyingi sana

Je, haikuwa Kiu ya maji?

Nawatakia Dominica Njema!
 
Kama wao wamesoma theolojia na sisi waumini wao hatukusoma watutafsirie tu. Ila na sisi tukisoma theolojia itakuwa shughuli pevu kututafsiria
 
Mchungaji ambae kweli anamjua Mungu anaongozwa na Roho Sasa je wewe una Roho ya Mungu [emoji16]
Mchungaji mda wote anajiweka karibu na Mungu hivyo ni rahisi kuwepo uweponi mwake wewe mda mwingi unaenda kwenye mishemishe
 
Imekuwa ni kawaida Wachungaji kutafsiri Neno la Mungu ( Injili) Wakati wa mahuburi

Lakini Biblia imeandikwa kwa Lugha inayoeleweka

Mfano Yesu baada ya kutembezwa umbali mrefu na baadaye kusulubiwa msalabani alisema " naona Kiu"

Sasa hii kauli ya " naona Kiu" imekuwa na tafsiri nyingi sana

Je, haikuwa Kiu ya maji?

Nawatakia Dominica Njema!
Wewe utatafsiri visivyo kweli. Kuna waliosomea biblia kuitafsiri, kama walivyo mahakimu, majaji, lawyers etc etc! Kwenye Sheria.
 
Unaposoma Biblia Usichukulie poapoa kama vile unasoma Gazeti kile kitabu kina mambo mengi ya kujifunza pia inahitaji umpate mwalimu mzuri ambaye anayeweza kukufunulia kile kilichoandikwa, ukitumia akili yako uwezi uelewa mafunuo ya Biblia
 
Kwani anayetafsiri anatumia akili ya nani?
Inahitaji maongozo ya Roho wa Mungu kukuongoza kwenye usomaji wako,ndio maana kabla ya kusoma inahitaji kumuomba pia Roho mtakatifu akusaidie kuweza kukufunulia lile Neno unalolisoma na pia uweze kulipokea na kuliamini pia sababu ni mara nyingi unaweza ukasoma na usielewe chochote hii pia utokea ndio maana tunahitaji kujizoesha kusoma sana na kutafuta kuyajua mafundisho ya kweli la Neno la Mungu ili uweze kukua kiroho

Ndio maana kuna u tofauti sana kwa yule aliye mchanga kiroho na yule aliyekuwa kiroho kwenye uelewa
 
Back
Top Bottom