JE, NI SALAMA KIAFYA KULA ASALI ILIYOPIKWA???

2017 No Name

Senior Member
Joined
Jul 26, 2017
Posts
172
Reaction score
133
Siku chache zilizopita nilipewa asali lita tano kama zawadi. Baada ya kugawa baadhi kwa jirani zangu nikabakiwa na lita ka 3. Niko pekeangu so nikawaza ntawezaje kuitumia hii asali iishe. Nikagundua kua nnaweza kuacha kuweka sukari kwenye uji nikaweka asali. Baada ya kujaribu nikaona uji una ladha nzuri tu. Ni uji wa lishe, nilikua naweka blueband na sukari now naweka blueband na asali.

Moja ya jirani zangu baada ya kumwambia huu ulaji akanambia NIACHE kuweka asali kwenye vitu vilivyopikwa, ina madhara kiafya. Kwa madai yake asali ikipata moto baadhi ya vitu vilivyomo katika asali vinageuka vinakua sumu (inaitwa HMF nini nini sijui) and pia baadhi ya vitu vinatengeneza aina ya gundi ambayo ikiingia tumboni haiwezi kuyeyushwa na mfumo wa chakula hivyo inaganda kwenye kuta za tumbo. Na hii gundi ikishajitengeneza hamna jinsi ya kuitoa na inasababisha matatizo ya tumbo.

Nimejaribu kugoogle ila sjaona sehemu yoyote waliyoandika kuhusu hii mada kwa kiswahili. So naomba mnisaidie wataalamu wa asali, Je,kula asali iliyopikwa pamoja na chukula au kuchanganywa na chakula chamoto kuna madhara???
 
Sidhani kama kuna madhara ila tusubiri wataalam
 
Haina madhara ,na tena hata kwenye chai weka asali changanya na mdalasini ni tiba nzuri Sana achana na ma bush doctor hao
 
Usiweke asali kwenye maji ama chakula cha moto kwasababu mbili

1) Unaua nguvu yote iliyopo katika asali pamoja na nutrients ambayo ni dawa zaidi ya 300. Ukiweka utapata utamu ndio ila hutapata virutubisho haswaa vya asali.

2) Ukiweka asali kwenye maji ya moto (sijui kwenye chakula) omba usijikwae kidogo kwa muda huo, unaweza kuvunjika kiutani sana na hii inawakuta sana madogo wanaokimbiakimbia na kucheza hovyo. Ni kwasababu asali ukiweka kwny maji ya moto na kutumia inalainisha sana mifupa huwezi amini.

Binafsi tangu nikiwa mdogo siwezi kukosa asali mbichi na tangawizi ndani...tena nakula hivyohivyo ikiwa mbichi.
 
Duuh, mwaka wa 7 huu natumia asali kama mbadala wa sukari- sikuyajua hayo. Nitafuatilia
 
Around the world most traditional medicine practices agree that heated honey has a negative affect on the human body. In the case of ayurveda, it is believed that honey heated over 60 degrees celsius (140 degrees fahrenheit) creates “ama”. Ama is a condition of mucus that is brought on by inflammation and toxicity.Nov 19, 2013
Source :Google
 
Blue Band ndio sumu. Nitaelezea kwa kirefu kwenye uzi mwingine. Ila Blue band ni sumu kali sana haya inzi hagusi Blue Band. Iweke sehemu anapofika inzi au panya. Utaona inzi au panya haguzi hio sumu
 

Nimekuelewa,.. so ni kwamba virutubisho vinaondoka tu ila haiwi sumu???
 
Blue Band ndio sumu. Nitaelezea kwa kirefu kwenye uzi mwingine. Ila Blue band ni sumu kali sana haya inzi hagusi Blue Band. Iweke sehemu anapofika inzi au panya. Utaona inzi au panya haguzi hio sumu

Sijawahi kujua,.. unaweza tuelezea japo kwauchache???
 
Mi ndio nasikia leo,na hiyo kuweka kwenye chai ndio ulikuwa mchezo wangu,sasa kama ni kweli sijui kama ntasalimika..
 
Blue Band ndio sumu. Nitaelezea kwa kirefu kwenye uzi mwingine. Ila Blue band ni sumu kali sana haya inzi hagusi Blue Band. Iweke sehemu anapofika inzi au panya. Utaona inzi au panya haguzi hio sumu
mkuu unataka kusema vitu visivyoguswa na inzi au panya ni sumu kwakua wao hawali? mbona mafuta yanayopatikana kwa maziwa ya ng'ombe ni sumu kwa ng'ombe mwenyewe lakin kwetu ni salama.?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…