Je, ni sawa kwa watu wazima kutazama Cartoons?

Mkogoti

TAPELI Mkubwa
Joined
May 3, 2020
Posts
2,415
Reaction score
3,924
Mtu Mzima (18+) kutazama katuni ni SAWA? Au ni ukosefu wa kazi za kufanya?

Toa Mtazamo wako.
 
Mkuu inategemea na mazingira aliyelelewa/aliyokulia Kuna jamaa anaweka mpaka what's up status za katuni Ila jamaa ni wakishua sana na ameishi Sana nje mpaka wazazi walipo staafu kazi na kurejea tz .
 
Inategemea na cartoon yenyew, me naangalia tom and jerry, frozen n.k.
 
Mim adi kesho YouTube yangu recommend videos ni cartoon.. napenda katuni tangu nipo mdogo adi leo na uzee huu.. since 2000. Katuni ni hulka ktk makuzi
 
Cartoon ni mtiririko wa story kama zilivyo sinema nyingine kwa hiyo si mbaya kama unaelewa story
 
Tom and Jerry unaiachaje hii???

acha utani
 
Kila mtu na maamuzi yake au unataka waangalie ponografia?
 
Me ni mtu mzima ila natazama baadhi ya katuni tena fresh kabisa. Tuache kucomplicate sana mambo wakuu.
 
Kila mtu afanye vile inavyompendeza....kuna watu wanaamini kuangalia movie yoyote ni ukosefu wa kazi, wapo wanaoamini kuanzisha uzi ni ukosefu wa kazi...utaacha kufanya yote kwa sababu ya binadamu?
 
watu wazima nao si walikua nao watoto si mbaya kujikumbushia
 
Mkuu nisikufiche Nina miaka 37 sasa lakini kila siku nakaa na watoto wangu watatu sebuleni tunaangalia katuni na sioni ajabu kama kitu kilichonikuza toka udogoni kwangu na kunipa furaha eti uzeeni niache nakueleza tu nasubiri mpaka wajukuu nitakaa nao tutaangalia katuni.

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Huwa siwezi kuangalia movie kama nna katuni ambayo sijaitazama, napenda sana katuni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…