Kuna makundi aina tatu ya watu wenye kupinga uchawi. Wapo ambao wao wanapinga na kusema kabisa kuwa hakuna uchawi, wapo ambao wanapinga uchawi kwa sababu hawajawahi kushuhudia hiyo nguvu ya uchawi zaidi ya kusikia tu kuna muda watu hawa hukubali uwepo wa uchawi pale itokeapo kushuhudia hiyo nguvu ya uchawi, lakini pia wapo ambao wanaamini kuwepo uchawi ila si kitu ambacho hukihusisha kwenye maisha yao ya kila siku na pengine huona kuna uwongo mwingi kuliko ukweli.Watu wameamua kuukumbatia uchawi ila ki uhalisia hiyo dhana haina tija yoyote!
Sawa mkuu asante kwa maoniKuna makundi aina tatu ya watu wenye kupinga uchawi. Wapo ambao wao wanapinga na kusema kabisa kuwa hakuna uchawi, wapo ambao wanapinga uchawi kwa sababu hawajawahi kushuhudia hiyo nguvu ya uchawi zaidi ya kusikia tu kuna muda watu hawa hukubali uwepo wa uchawi pale itokeapo kushuhudia hiyo nguvu ya uchawi, lakini pia wapo ambao wanaamini kuwepo uchawi ila si kitu ambacho hukihusisha kwenye maisha yao ya kila siku na pengine huona kuna uwongo mwingi kuliko ukweli.
Sasa shida nyengine humu zile imani potofu za watu ndio hutumika kama kigezo cha kuonyesha kwamba hakuna uchawi bali ni ukosefu wa elimu na uelewa wa watu, kitu ambacho sio sahihi maana imani potofu ziko hadi katika mambo mengine pia.
Kwahiyo mimi bado nasisitiza kama hicho kinachoitwa uchawi ingekuwa hakina matokeo basi imani ya uchawi ingekuwa ishaisha.
Kwanini wewe usiende kwa mganga kumroga mtu kisha uone matokeo yatakuaje?Anayeweza kuniroga nimemruhusu akaniroge na alete ushuhuda hapa.
Hakuna uchawi bali utapeli.Kwanini wewe usiende kwa mganga kumroga mtu kisha uone matokeo yatakuaje?
Mkuu ukitaka kuzungumzia utapeli kwenye imani za kichawi tunaweza kuzungumzia ila pia ukitaka kuzungumzia uchawi pia tunaweza kuzungumzia, tusichanganye mambo mkuu maana utapeli upo kila mahali.Hakuna uchawi bali utapeli.
Kwangu uchawi na utapeli havitenganishwi.Mkuu ukitaka kuzungumzia utapeli kwenye imani za kichawi tunaweza kuzungumzia ila pia ukitaka kuzungumzia uchawi pia tunaweza kuzungumzia, tusichanganye mambo mkuu maana utapeli upo kila mahali.
Ni kwa sababu wengi wenu humu uchawi ni kitu mnachokisikia zaidi kuliko kushuhudia, wengi humu mnazungumzia story za utapeli wa waganga, imani potofu ambazo mnazisikia zenye kuhusishwa na uchawi. Kwahiyo kama uelewa wako kuhusu uchawi ni kupitia hizo story za utapeli basi ni wazi lazima ushindwe kutenganisha.Kwangu uchawi na utapeli havitenganishwi.
Usibishane nao list yao ninayo hapa inafanyiwa uhakiki ili mgao ufike kila kayaNi kwa sababu wengi wenu humu uchawi ni kitu mnachokisikia zaidi kuliko kushuhudia, wengi humu mnazungumzia story za utapeli wa waganga, imani potofu ambazo mnazisikia zenye kuhusishwa na uchawi. Kwahiyo kama uelewa wako kuhusu uchawi ni kupitia hizo story za utapeli basi ni wazi lazima ushindwe kutenganisha.
Mgao wa niniUsibishane nao list yao ninayo hapa inafanyiwa uhakiki ili mgao ufike kila kaya
Genz mna vituko sana.Nimewekea rejea ya vitabu vya dini kwa kutaka kuonesha kua hii dhana ya uchawi ni ya kale
Ajabu yake huko vitabu vya dini na imani vilipoanzia hawajishughulishi na hii dhana ya uchawi kama huku africa
Kama unaweza kufanya mtu akupende na akakupenda je hakuna namna mzazi anaweza kufanya kutumia huo uchawi mtoto akashika no moja darasani
Yaani kwa faida maana umesema wanafaika wa uchawi ni wachawi wenyewe
Alieunda uchawi alikua hopeless kaunda kitu hakina manufaa zaidi ya uharibifu tu
Mimi binafsi nikitaka kujiunga na wa chawi ili nipate hiyo cheap ya usafiri nawezaje?
Kikundi cha kikuda hiki hakina faida yoyote
Uko sahihi,,,,,Hello jamii intelligence 👋
Wakuu hii habari ya uchawi nadhani sio jambo geni
Uchawi ulitajwa kwenye vitabu vya dini hasa hivi maarufu Bible&Qur'an
Kwa bible mfano Kutoka 22:18 inasema:
Usimwache mchawi kuishi
Huu ni ushahidi kua Bible inatambua uchawi
Uchawi umetajwa pia kwenye Qur’an, hasa Al-Baqarah 2:102 ambapo inazungumzia habari ya uchawi na watu kujifunza mambo hayo
Huu nao ni ushahidi Qur'an inatambua habari za uchawi
kwa mantiki hii dhana ya uchawi ni ya kale sana
Huku Africa watu bado wamekumbatia hii imani sana, sijui huko Ulaya ikoje
Utasikia mtu anasema
👇
Mtoto huyu karogwa, sio akili zake.
Hapa tunaona uchawi unatajwa kama kitu ambacho kinaweza kubadilisha hali ya mtu
Alikuwa mzima, ghafla akawa kichaa au mtu asie sawa kama alivyokua kabla
Mtu anaumwa, unaambiwa karogwa
Sasa najiuliza...
Uchawi umetengenezwa au umeundwa kwa kufanya vitu negative tu?
Hakuna namna huo uchawi kama upo unaweza kutumika kwa njia positive?
Yaani tukaamua kutumia akili ya mtu kilaza akawa genius, kama vile inavyoaminika kwamba uchawi unaweza kumbadilisha genius kuwa kilaza?
Kuna hii pia👇
Ooh, wachawi wanapaa usiku...
Kwanini sasa kama hiyo technology ipo tusiitumie kupunguza foleni?
Huo usafiri wa kupaa uwe official sasa
Nyie wachawi wa JF(jokes)
haiwezekani kuwa hivi yaani huu uchawi ukawa na tija?
Hivi uchawi unafanya kazi kweli au ni mambo ya nadharia tu?
Niliwahi kua na matatizo ya kupata maumivu ya kicwa nakizunguzungu
Basi kuna mtu akamwambia mama:
Huyu ShesRise_1 amelogwa asifanye vizuri shuleni na si haba shuleni nilikua najitahidi kwahiyo huyo mama akamuambia mama angu huenda nimelogwa ili nirudi nyuma kimasomo🤔
Heh! 🤔
Nikastuka
Nikawaza, haya yatakuwa mambo gani?
Basi nikaanza kufanyiwa zile zinazoitwa tiba za Kisunna, visomo na mambo mengine
Ajabu ni kwamba kuanzia pale ndiyo kwanza nikaanza kupata maruerue.
Usiku naogopa kulala mwenyewe.
Naota ndoto za ajabu, heh... tafrani mtindo mmoja
Kumbe ile issue ya kuanza kuota mauza uza ni kwa sababu
ya saikolojia bana
Yaani saikolojia kwa maana baada ya kusikia nimelogwa na kupelekwa kwenye visomo
Ndiyo ubongo ukaanza kuniundia mapicha picha
So nilivyoambiwa tu vile, akili yangu na ubongo wangu vikaanza kujishughulisha na hayo mambo
Mara nione hiki...
Mara nisikie kile...
Mara nianze kujiuliza, Hivi huu ni uchawi gani?
Asieee!
Nikakaa nikasema:
Hapana, hizi mbona kama fix?
Na mimi by nature nina kaubishi fulani sipendi kumezeshwa mambo japo mwanzo wali ni win
Nikaacha kabisa huo upuuzi
Nikaamua ku-clean akili yangu
Kuanzia hapo nikiambiwa
Njoo kwenye visomo
Nawaambia
Mimi sina tatizo lolote
Na kweli, nilifanya vipimo hospitali nikambiwa kicwa kilikuwa kinauma kwa sababu sikuwa na damu ya kutosha, na ndiyo maana nilikuwa naumwa kicwa na kizunguzungu
Na hata sijui ilikuaje na mama akaingia kwenye mtego wa rafiki yake akaacha kunipeleka hospital kwanza akaanzia kwenye imani huku
Nikatumia zangu dawa nikawa fresh
Sijaumwa tena kicwa, labda cha mafua tu
Sioni mauza mauza wala nini
Naishi vizuri kabisa
Ndipo nikaja kugundua kumbe mambo mengine ni saikolojia tu
Wala hakuna cha uchawi wala nini
Na kuna hii pia ya majini kutaja uchawi bila majini sio sawa ni mtu na shoga yake
Sasa imagine eti mtu anapandisha mashetani anataka dhahabu...
Heh! Dhahabu sasa inatoka wapi yani?
Mashetani wana migodi yao huko?
Nimetoa mtazamo wangu kuhusu hii dhana ya uchawi
Je, uchawi ni nguvu halisi?
Au wakati mwingine tunaita kitu uchawi kumbe kuna sababu za kiafya, kisaikolojia au mazingira ambazo hatujazijua?
Na kama kweli uchawi una uwezo wa kumbadilisha mtu kutoka kuwa genius mpaka kilaza...
Kwanini usitumike kinyume chake?
Au kama wachawi wanaweza kupaa...
Kwanini bado tunakaa kwenye foleni?
Kama hii dhana ya uchawi haina tija kwanini tuna ing'ang'ania?
ShesRise_1 ✋️
Mchawi anacheza vp na saikolojia yako ilhali mchawi huwa hajitangazi kuwa yeye ni mchawi kama wafanyavyo waganga?Uchawi ni saikolojia. Wachawi & waganga hucheza na saikolojia zetu
Sawa mkuu huvunji sheria so hakuna tabuMimi ninaamini Mwenyezi Mungu yupo, nguvu zake zipo na ni halisi na pia Wachawi, Washirikina na Majinn yapo.
Kama uwezekano huo upo basi lift nipeweGenz mna vituko sana.
Kwa hiyo unataka kuwapanga wachawi wawe wanakupa lift ya usafiri kwenda Town
Eeh ni issue za saikolojia ukiambiwa umerogwa hapo hapo unaanza kuona mauza uza wakati kabla ulikua huyaoniUchawi ni saikolojia. Wachawi & waganga hucheza na saikolojia zetu
Nendq kaishi Sumbawanga vijijini au Gamboshi halafu uwaambie wazee kwamba"uchawi hakuna ni mambo ya kisaikolojia tu" halafu sikilizia matokeo ndani ya mwezi mmoja utapata majibuEeh ni issue za saikolojia ukiambiwa umerogwa hapo hapo unaanza kuona mauza uza wakati kabla ulikua huyaoni
Huko ndiyo makao makuu ya uchawi?Nendq kaishi Sumbawanga vijijini au Gamboshi halafu uwaambie wazee kwamba"uchawi hakuna ni mambo ya kisaikolojia tu" halafu sikilizia matokeo ndani ya mwezi mmoja utapata majibu