Je, ni uchawi au saikolojia?

Wallah nahisi ni chai kaka 😅
Mpaka nione kwa macho yaani
Sasa hivi maendeleo ya vitu, watu kustaarabika na mabadiliko ya kizazi hayo mambo ni ngumu kuyaona au kuyashuhudia. Lakini hizi mambo zimebakia kuwa history tu.
 
Lakini hiyo story ya Bibi kujigeuza fisi sio Chai ni kweli kabisa .😃😃😃
 
Sasa hivi maendeleo ya vitu, watu kustaarabika na mabadiliko ya kizazi hayo mambo ni ngumu kuyaona au kuyashuhudia. Lakini hizi mambo zimebakia kuwa history tu.
Sitakiii kuamini kaka😌
 

Ulichokieleza kuhusu maumivu ya kichwa na sababu za kiafya ni sawa: si kila tatizo ni uchawi, na ni muhimu kutafuta sababu za kiafya kwanza. Lakini Biblia na Qur’an hazisemi kwamba kwa sababu baadhi ya mambo yanaelezeka kisayansi au kisaikolojia, basi uchawi haupo kabisa.

Biblia:

Kutoka 22:18 inasema: “Usimwache mchawi kuishi.”
Hii yenyewe inaonyesha Biblia haikuchukulia uchawi kuwa hadithi tupu.

Pia Matendo 8:9-11 inamtaja mtu aliyeitwa Simoni ambaye alikuwa akifanya uchawi na kuwashangaza watu. Na Matendo 16:16-18 inasimulia msichana aliyekuwa na “pepo wa uaguzi” na watu walipata faida kupitia utabiri wake.

Qur’an:
Al-Baqarah 2:102 inasema kuhusu watu waliofundishwa uchawi na hata inaeleza kwamba uchawi huo unaweza kutumika kuleta madhara, kama kutenganisha mtu na mwenzi wake. Qur’an pia inasema:

Al-Falaq 113:4: “Na kutokana na shari ya wanaopuliza mafundoni.”

Kwa hiyo Qur’an haikanushi kuwepo kwa uchawi; inatuonya dhidi ya shari yake.

Lakini kuna jambo muhimu: Biblia na Qur’an hazifundishi kwamba kila ugonjwa, kila kushindwa shuleni, kila ndoto au kila tatizo ni uchawi. Huwezi kuchukua mfano wa mtu aliyegundulika ana upungufu wa damu, kisha ukatumia huo kuthibitisha kwamba uchawi wote haupo. Huo ni kama kusema, “Baadhi ya watu hudhaniwa wamepagawa lakini kumbe wana ugonjwa, kwa hiyo mapepo hayapo.” Hiyo haifuati.

Na swali lako la: “Kama uchawi upo, kwa nini usitumike kufanya genius awe genius zaidi au kupunguza foleni kwa kupaa?” — hilo ni dhana yako kuhusu uchawi, si mafundisho ya Biblia wala Qur’an. Vitabu hivyo havisemi kwamba uchawi ni teknolojia yenye matumizi yoyote tunayoyataka. Vinauhusisha na mambo ya siri, udanganyifu na madhara.

Hata Biblia inatofautisha uchawi na miujiza ya Mungu. Kwa mfano, Kutoka 7:11-12 inataja waganga/wachawi wa Misri waliweza kufanya mambo yao, lakini nguvu zao hazikuwa sawa na uwezo wa Mungu.

Kwa hiyo hoja sahihi si: “Kwa nini mchawi hapandishi watu angani?”
Hoja sahihi ni: Biblia na Qur’an zote zinatambua uchawi kama jambo lililokuwepo, lakini zinakataza kuufuata na kuutumia. Na pia si sahihi kuita kila tatizo la kiafya au kisaikolojia “uchawi.”
 
Nani alianzisha uchawi ?
Alikusudia nini?
Tuanzie hapa ili twende taratibu
 
Ila katika kitu chenye kunishangazaga humu kuhusu watu wenye kudai hakuna uchawi ni kwamba ukijadiliana nao humu unaweza kusema hawa jamaa wote hawaishi africa, yani kana kwamba toka utoto wao hadi utuuzima hawana experience yoyote na matokeo yenye kuhusu na uchawi katika maisha yao hivyo ni kama unajadiliana na watu waliyozaliwa na kukulia nchi za ulaya huko ambako uchawi kwa kiasi kikubwa ni kama masimulizi tu.
 
Nimezaliwa Africa na nimekulia hapa pia sijawahi kuona mama yangu akitupeleka kwa waganga zaidi ya hicho kipindi alivyoambiwa na rafiki yake na alinipeleka kwa sheikh tu sijawahi kuona tukiogeshwa madawa wala kuchanjwa sijawahi kuona athari yoyote kuhusu uchawi achilia mbali faida
 
Wala sijazungumzia faida,hasara wala ukweli na uongo hapo mkuu. Ulaya tunajua kule idadi ya watu kuamini uchawi ndogo na hiyo hupelekea kutokuwa na matukio yenye kuhusishwa na uchawi ama watu kujihusisha na matendo yenye kuaminika ni uchawi.

Sasa humu watu wenye kueleza experience zao kwenye mambo yenye kuhusishwa na uchawi ni watu wenye kuamini uchawi tu ila wenye kudai hakuna uchawi wao hawajawahi hata kushuhudia hayo matukio yenye kuhusishwa na uchawi yani hawajawahi hata kusikia tu matukio hayo hata kwa ndugu ama rafiki zao.

Na hapo ndipo panapo nishangaza, najiuliza wote tunaishi afrika hii hii ama?
 
Tupo hapa hapa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…