Je ni uoga tu au kuna la zaidi?

naungamkono hoja... nadhani haijalishi kama watu wanakaa mbali au karibu... periodic testic ni nzuri hasa kwa watoto na couples wenyewe kwani wanweza kujipanga zaidi na hata kuepusha maabukizi zaidi (kama yapo)

cha maana sasa ni advocacy na uamsho wa ziada watu kukubali kupima. Now the question still lingers; hivi ni kweli kwamba wanaohitaji sensitization ni wanaume pekee?

Je kwanini tusiweke sheria kwamba kupima ni lazma?

Kuna mradi wa PITC (provider initiated testing and counselling)... hapa nadhani tungetilia mkazo kiasi kwamba hata kama unaenda kutibiwa kidonda uwe unapata test; watoto wa nursery wote wapimwe ili kujiandaa kuwalea vizuri na hata wanaotafuta medical clearance nao wapimwe... mwanzo utakua mgumu lakini baada ya 2 years tutazoea tu
 
 

hahaha jibu lako limenivutia
endelea kuwa makini The Boss
ABC naona unazifata vizuri
 
MJ1, wakati tukifikiria along those lines, unakumbuka kiapo cha ndoa? cha kwanza ni UAMINIFU!!

Ni kweli inatupasa kukumbuka kiapo lakini Kaizer reality inaonyesha kuwa wengi hatuzingatii kiapo hiki-otherwise UKIMWI ndoani ungekuwa ni hadithi ya kuisikia tu. Tusifumbie macho reality jamani kisa kiapo. Mimi nawakumbusha uaminifu siku hizi hakuna dunia imebadilika. Nina mifano hai mingi tu ambapo mke/mume amemletea mwenzake huu ugonjwa pamoja na kuwa walikula kiapo.


Sio Ukapime Kaizer- tukapime. Ndio maana nikasema tukishawezakuifanya kuwa utaratibu wa kawaida ndani ya nyumba sidhani kama italeta hisia tofauti. Kumbuka wewe unawezakuwa umejitunza but mie nikateleza so usiniamini kihivyo love kwa ababu kosa likitokea ni la maisha si kuwa unaweza ku-undo.


yeah tulishajiandaa, lakini tulimhonga kwanza MC apeleke mambo chap chap..shangazi tukamweka sawa kabla.....afu mshenga alikuwa na desa la maswali...lol mambo mswano!

hapo Blue I hope Kova hajaiona maana siku hizi yeye ndo TAKUKURU. Am happy kama kila kitu kilikwenda sawa bin sawia
 
 
hope uliniwakilisha kwenye sendoff ma luv.....hii nguo c ndio tulicmama nayo altareni cku zile... remember?

yes babe, I remember....ngoja nikdediketia kawimbo leo....

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=YjUaWiy_QXc[/ame]
 
hahaha FL1, unadhani hajitambu ki ivyo hadi akatambuliwe na vitambuzi vinavoweza kukutambua vinavyotambua vyenyewe? LOL

Anaweza kuwa hajitambui bwana ..unaweza banjuka mala moja ukaukwaaa na pia inawezekana ukabanjuka more than a million lakini usiukwae
Epuka kuchangia ,Mikasi ,Wembe ,....nk nk
 
 
 

Hapo juu nakubaliana na wewe moja kwa moja luv,lakini essense ya sredi tangu mwanzoni haikuwa ivo,,hebu angalia hapa chini,

Sasa hivi mjadala unaweza kuwa balanced kwa maana ya kwamba labda uedit bandiko la mwanzoni kabisa ambalo ni:

 

Ki ukweli sio sahihi kabisa kwa mpenzi wako ambaye mko nae mbali kukuomba ukapime HIV. Yani akikwambia hivyo siku moja jua amekosa imani na wewe!
 
Kwani wanawake ni wepesi wa kwenda kupimwa virusi? Naombeni takwimu tafadhali....
 
Mie bado nachezaga Chagulaga siendi pima sasa
 
Ki ukweli sio sahihi kabisa kwa mpenzi wako ambaye mko nae mbali kukuomba ukapime HIV. Yani akikwambia hivyo siku moja jua amekosa imani na wewe!
Napata shida kweli hapa hasa nikifikiria risk tunayocheza nayo in the name of UAMINIFU upo ndani ya ndoa!! Mi jamani nikifikiria kukiacha kibaby changu huku nisijue kinalelewaje inaniuma sana unless tuseme sasa tumeamua kuuchukulia ugonjwa huu kama malaria tu kuwa upo na ukiupata its part of life (Sisemi kuwa ukiupata ni kifo la hasha kwani najua kuna wanaoishi hata baada ya kuupata but jamani kama tuna uwezo wa kuzuia kwa nini tusizuie?


Tujenge mazoea ya kupima wapendwa yaani iwe among out life's menu please
 
Kwani wanawake ni wepesi wa kwenda kupimwa virusi? Naombeni takwimu tafadhali....

Hakuna sehemu inayosema kuwa wanawake ni wepesi kupima UKIMWI mimi nimeiweka hivyo kwa kuwa kuna thread ilishawahikurushwa juu ya upimaji wa DNA kwa wenetu na ikaonyesha kuwa wanaume walikuwa so possitive kwenye kupima DNA ndo nikauliza why uwepesi huu usiwe na kwenye VVU/UKIMWI?
 
Hao ni waoga tu,

UKIMWI tukapime wote ili tufanye comparison ya majibu, kama mimi ni -ve naye ni +ve itakuwa ni habari njema tu.

DNA, mnh.
 

Lakini MwanajamiiOne, kupimwa virusi na kupima dna kuhakikisha kama kweli mtoto ni wako ni vitu viwili tofauti ingawa vyote ni vya muhimu. Hebu jiweke ktk nafasi ya mwanamme ambaye kadanganywa na kubambikiwa mtoto asiye wake halafu akamlea na baadaye kuja kugundua kuwa si wake? Utajisikiaje kama ni wewe? Hakuna mtu ambaye anapenda kutwishwa jukumu ambalo si lake na ni kutokana na udanganyifu wa baadhi ya wanawake ndio maana baadhi ya wanaume wanakuwa wepesi kuomba upimaji wa dna kufanywa ili wahakikishe kweli majukumu yaliyopo mbele yao ni yao kweli. Na hilo halina ubaya wowote na mwanamke kama ana uhakika baba ni nani wala hatabisha wala kusita kwenda kupima. Tunaishi kwenye dunia ya kutokuaminiana siku hizi.
 

MJ1,

Kwani inachukuwa muda gani kuambukizwa HIV au kupata mimba nje ya ndoa?

HIV au mimba is a matter of minutes and not hours or days! So kama unawasiwasi na mwenzi wako kiasi hicho inabidi mpime kila siku kabla ya kufanya tendo la ndoa. Believe me, kama ni fisadi wa ngono anaweza kwenda kazini asubuhi akiwa mzima (HIV -ve) lakini akirudi nyumbani jioni ni HIV +ve!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…