Je ni uoga tu au kuna la zaidi?

mwe!!😕
 
Baby I know but hata nikipima mimi peke yangu does it mean tuko salama? Inawezekana nikawa carrier na nimekuambukiza wewe switii. Loh leo kazi ipo!!

Na kumwambia wife twende tukacheck DNA hutilii shaka uaminifu wake kwenye ndoa?
 
Mi nadhani hapo inawezekana uposahihi...u need some rest my dear....halafu ufanye reflections

Kaka yaani niache tu

Najaribu kufikiria iwapo UKIMWI ungekuwa unaambukizwa kwa kunywa maji ingekuwa rahisi hata kuwashauri watu wakapime maana uwezekano kuwa maji ya chupa si salama wangeamini maana ni wengi wanakunywa maji hayo.
 
Kwa maelezo yako hapo juu hii thread iko nje ya viwanja vyako. Hapa wanaongea wale ambao wanacommitment za ndoa na siyo wale wa "bado nipo nipo kwanza" kama wewe. Maisha ya ku-date ni too artificial. Na kama huwezi kubeba risk ya kumwamini mtu ambaye umejikabidhi kwake basi hii kitu umekukalia kushoto. Labda siku nyingine utatusasidia sana tutakapohitaji uzoefu wa cheating kwenye mahusiano yasiyo ya kudumu. Kwenye ndoa ni ama unaamini au unaishi kwa kizunguzungu kama anavyoeleza MJ1..
 
We Omega Psi Phi utaruka ruka nje mpaka lini? Unataka nywele nyeupe mkichwa ndo ufunge pingu?
 
vinasaba = DNA, kazi kweli kweli
 
Hii thread ina progress na kupanuka kama zilivyo thread/mada zingine.

Halafu unasema maisha ya ku-date "ni too artificial"....nini kilicho genuine ktk maisha ya ndoa kama mambo yenyewe ni nyumba ndogo na kuleteana migonjwa na kubambikiana watoto?
 
We Omega Psi Phi utaruka ruka nje mpaka lini? Unataka nywele nyeupe mkichwa ndo ufunge pingu?

Hehehehehee...wewe Fideli wale waliooa na kuolewa lakini bado wanarukaruka wana tofauti gani na mimi? Na usisepe....nijibu swali langu.
 
Hii thread ina progress na kupanuka kama zilivyo thread/mada zingine.

Halafu unasema maisha ya ku-date "ni too artificial"....nini kilicho genuine ktk maisha ya ndoa kama mambo yenyewe ni nyumba ndogo na kuleteana migonjwa na kubambikiana watoto?

Nasema hivyo kwa sababu ni transition. Hakuna kitu real kwenye kipindi cha mpito. Pita kwanza ndo ukane na vitu vyenywe. Hiyo (blue) ndiyo real life. You either live it or run away (if u can)!
 
Nakuelewa, lakini kama unataka kujua HIV status, kwa msingi wa hayo niliyoyasema si inaweza kubadilika within minutes tu? Si lazima mtu awe hayupo kwa muda mrefu (masomoni, kikazi etc) ndio anaweza kuwa ameambukizwa!

Kupima kwa maana ya kupanga maisha ni jambo jema. Lakini kama ni precaution ili mwenza asikuambukize sidhani kama inawezekana kwa maisha ya kawaida ya ndoa. Ni vizuri wanandoa wakaenda kupima HIV pamoja lakini kama mmoja hayupo tayari, si vema kumlazimisha (Unless kama unasuspect alikuwa exposed mahali, in which case itatakulazimu umwambie ukweli kuhusu wasiwasi wako!).
 
Nasema hivyo kwa sababu ni transition. Hakuna kitu real kwenye kipindi cha mpito. Pita kwanza ndo ukane na vitu vyenywe. Hiyo (blue) ndiyo real life. You either live it or run away (if u can)!

What do you mean pita kwanza ndo ukane vitu vyenyewe? Na sikuelewi kabisa....unasema hakuna kitu real kwenye kipindi cha mpito? WTF.....what's real about cheating on your wife or husband?
 
Exactly. Ndicho ninachosema hapa wajameni......sababu hasa ndiyo italeta maana na nia ya wewe 'kumshauri' akapime.

Lakini sababu yenyewe ikiwa ni eti kwa vile ulikuwa mbali , masomoni, etc, hiyo kwangu haitoshi na inaspell kitu kimoja tu kuwa HUNIAMINI. Na kama huniamini hakuna sababu ya kujifanya kuendelea kuishi kama MUME na MKE. narudia tena UAMINIFU kwa maana ya Dark City ndo msingi wa ndoa wajameni, kama hamuaminiani kwa vile tu wanandoa siku hizi wanaongoza kwa virusi, kwa nini tuoane? tuvunje tu ndoa
 
Hehehehehee...wewe Fideli wale waliooa na kuolewa lakini bado wanarukaruka wana tofauti gani na mimi? Na usisepe....nijibu swali langu.

Natamani nilete posa lakini inaonyesha wewe katili sana.
Wenye tamaa zao ndo hao wanaruka ruka ndo maana mm huwa nasema kama unapenda mnene oa na kama unapenda mwembamba oa au oa wote kwa pamoja si ruksa bana kikubwa maridhiano ukiona huyo bado hajaridhika anatoka nje basi ni kicheche.
 
What do you mean pita kwanza ndo ukane vitu vyenyewe? Na sikuelewi kabisa....unasema hakuna kitu real kwenye kipindi cha mpito? WTF.....what's real about cheating on your wife or husband?

Don't go too far. Cheating is everywhere; iwe kwenye uchumba au kwenye ndoa. Na siyo wote wanacheat ingawa watu wanaocheat wanasemekana ni wengi. I am not among them.
Ninachomaanisha ni kuwa kuishi single siyo suluhisho la ukimwi na other heart-breaking encounters. Huwezi kuipenda ngoma inayochezwa mbali na hata sauti zake husikii. Kaingie hadi kilingeni ucheze ili uwe na upande. Mimi ninao na ndiyo maana ninaongelea uzoefu wangu. Lakini sina maana kuwa hakuna watu wanaoumia kwenye ndoa kama vile ambavyo kuna wale wanaofurahia. Halafu kwenye ndoa hakuna suala moja tu la ukimwi na DNA. Yapo mengi tu. Ukijenga wasi wasi basi wewe pressure itakaa kwenye 150/120 mmHg milele and your days will be just numbered!
 
Natamani nilete posa lakini inaonyesha wewe katili sana.

Ulete posa kwetu? Heheheheheheeee.....samahani mimi napenda wanawake bana. Mtafute Bwabwa kama unapenda wanaume.....juzijuzi alikuwa anatafuta mpenzi hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…