Je, ni usajili Gani Simba tulipigwa?

Je, ni usajili Gani Simba tulipigwa?

Labani og

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
19,637
Reaction score
29,473
Mwanzoni mwa msimu Klabu ya Simba kupitia viongozi wake waliweka bayana malengo ya timu kuwa ni Nusu Fainali ya CAF Champions Leagu, kulirejesha taji la Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na lile la Azam Sports Federation Cup (FA).

Uzinduzi wa msimu ukaanza na Kauli mbiu ya 'We are Unstoppable' ambapo CEO wa wakati huo Barbara Gonzalez (@bvrbvra) akisema kuwa ''Hatuzuiliki, hatushikiki.''

Katika kuhakikisha hilo wanafanikisha Mnyama akaingia sokoni kufanya usajili.

Je, usajili wa Simba msimu huu ndiyo kikwazo cha kushindwa kufikia malengo waliyojiwekea..?

1> Dejan Georgevic (Mzungu)
2> Victor Akpan
3> Mohamed Quatarra
4> Nelson Okwa
5> Auqustine Okrah
6> Ismail Sawadogo
7> Nasoro Kapama
8> Habibu Kyombo
9> Moses Phiri
10> Saido Ntibazonkiza
11> Jean Baleke

1684952332905.jpg
 
Okwa hua nacheka sana, Hana kitu ni uvabaishaji tu.
Tukapangwa nae kugombania namba hakivile namshinda.
 
Hakuna usajiri waliopigwa bali walipata wachezaji kulingana na pesa yao ilivyokuwa....!!, Hata unapokwenda dukani kununua simu utakuta ya 3m na 1m automatically ukinunua ya 3m n Bora kuliko ya 1m. Kwa ufupi pesa yao ndio iliamua Aina ya wachezaji wanaowataka.
 
Back
Top Bottom