Je, ni vibaya kunyonyesha ukiwa mjamzito?

Nameless-

Member
Joined
May 21, 2009
Posts
47
Reaction score
1
Mwenye jibu la kisayansi anisaidie.

Kama mama ananyonyesha mtoto mfano mwenye umri miezi 9 na kuendelea, akipata ujauzito, kuna athari zozote kuendelea kunyonyesha mwanawe?
 
Hii mbona ni rahisi sana si ana acha tu kunyonyesha mkuu.
 
Haina uhusiano wowote mie kuna rafiki yangu alipata ujauzito huku ana mtoto wa miezi mitano akaenda kwa daktari wake kuomba ushauri, dr akamwambia hakuna tatizo basi kanyonyesha mtoto mpaka siku anaenda kujifungua, na hakukuwa na madhara yoyote watoto wote wana afya njema mpaka leo hii mdogo tayari ana miaka 2 na nusu.
 
Mama aendelee kunyonyesha na hakuna athari zozote.
 
Mwenye jibu la kisayansi anisaidie. Kama mama ananyonyesha mtoto mfano mwenye umri miezi 9 na kuendelea, akipata ujauzito, kuna athari zozote kuendelea kunyonyesha mwanawe?


Tumia nyota ya Kijani Nameless.

Shauri yako,

Utachekwa na mama mkwe!
 
Swali lako lina utata kidogo nimewahi kusikia kwamba sijui ukifanya hivyo unaweza bemenda mtoto..ila hilo sina uhakika nalo...ni vyema ukapata ushauri wa daktari.

Ila kuna kajiblog nimekaona leo kanaitwa; mashosti.blogspot.com

Ni kazuri kwa kina mama wajawazito unaweza kujifunza lolote
 
Wataalam,

MTOTO WANGU ANA UMRI WA MWAKA MMOJA NA MIEZI MITATU, MKE WANGU ANA UJAUZITO WA MWEZI MMOJA.

Je, kuna madhara yeyote ambayo mtoto anaweza kuyapata akinyonya katika kipindi hiki cha mabadiliko ya mwili sababu ya ujauzito?

Kama inaruhusiwa kuendelea kunyonyesha ni kwa mda gani?

Nashukuru sana.
 
Na mimi hili swali linanihusu, tafadhali tafadhali wataalam......
 
Kuna siku nilikuwa namsikiliza mtaalamu akasema wakati wa ujauzito mtoto anaweza kuendelea kunyonya hadi miezi sita au saba.

Ila kipindi ambacho mama amebeba ujauzitomwingine kunakuwa na mabadiliko ya homoni ambayo husababisha maziwa kuwa na virutubisho vingi na hivyo kusababisha mtoto anayenyonya kuweza kupatwa na tatizo la kuharisha, lakini ni kwa kipindi cha mpito tu yaani kipindi cha kushika mimba na baadae mtoto anaendelea kunyonya bila tatizo (kuna kasumba ya kusema mtoto amenyonya maziwa machafu ndo hicho kipindi cha mpito).
 
Kwa sasa mtoto anaharisha na kutapika, huenda ikawa ni sababu kuu. Nashukuru mkuu.
 
Kwa umri alipofikia mnaweza kufanya utaratibu wa kumuachisha ziwa la mama ili kupisha mabadiliko aliyo na kulinda afya yake.
 
Nakubaliana na wewe MKEMPIA. Mtoto wake BabaJunior anakaribia mwaka mmoja na nusu sasa. Bora amwachishe kunyonya tu.
 
Habari wana JamiiForums,

Mimi nimeoa na nimebahatika kupata mtoto mmoja ambaye mpaka sasa ana mwaka mmoja.

Sasa tatizo ni kwamba mke wangu ana mimba nyingine na bado mtoto wetu ananyonya.

Kiukweli sijui nini cha kufanya na ukizingatia mke wangu alijifungua kwa njia ya upasuaji mimba ya kwanza.

Naamini mtanishauri vizuri nini cha kufanya na wapi nianzie.
 
Mwachisheni mtoto kunyonya. Ila na wewe uwe makini bana watoto wapishane kidogo, sasa watakuwa kama mapacha bana!
 
Wadau,

Naombeni mnijuze kama kuna madhara yoyote kwa mtoto endapo mama atamnyonyesha huku akiwa na ujauzito mwingine.

Na je,ni baada ya kipindi gani mama anatakiwa kusitisha kunyonyesha akishajigundua kuwa ana ujauzito?
 
kwanza ilikuaje mpaka uwe na mtoto wa kunyonyesha afu upate ujauzito?:hurt::llama::llama:😡😡😡
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…