Hamza Nsiha
JF-Expert Member
- Jul 25, 2022
- 221
- 197
Ni dhahiri kuwa kuna vitu vingi ambavyo watu wengi huwa tunapenda kuvipuuzia lakina ki_uhalisia ni vitu vyenye kuleta athari kubwa katika afya zetu.
Baadhi ya vitu hivyo ni kama vile:
Baadhi ya vitu hivyo ni kama vile:
- Kukata matunda, na kuyaacha kwa muda fulani. Nadhani umewahi kukutana na sehemu ambazo wanauza matunda yakiwa tayari yamekatwa halafu yakawekwa katika vifungashio tayari kwa kuliwa. Endapo yataachwa kwa muda mrefu bila kufunikwa ni dhahiri kuwa yanaweza kupoteza virutubisho vyake ambavyo ni vitamini.
- Kupika mboga za majani mpaka rangi yake ya kijani kutoweka. Hii pia ni sawa na bure kwani virutubisho vyote muhimu hupotea kadri rangi yake inavyopotea.
- Kuongeza chumvi katika chakula wakati wa kula. Pia hili ni jambo ambalo tumelizoea lakini ni jambo hatarishi katika afya zetu.
- Utumiaji holela wa dawa za kutuliza maumivu kama vile paracetamol.