Je, ni wajibu wa Serikali kulinda aina na Quality ya vyakula vyetu

the power

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
407
Reaction score
799
Kibiashara ina make sense. Ingawa quality ya vyakula vyetu inakuwa compromised. Ebu tujaribu kudescribe baadhi ya matunda yetu kwa sasa, kwa kuanzia tu
:
1) Nanasi: Ili la kisasa ni kubwa balaa kama mpira, ila ukilikata unakutana na maji tupu, ule utamu wa nanasi umepotea kabisa, hakuna sukali unakula kama makapi. Likikaa siku mbili limeoza. Fikilia uliponunua nanasi hili Chalinze lilikuwaje

2) Tikiti maji: Yaani ili ndilo balaa, ukiondoa rangi nyekundu iliyoboreshwa , utatamani ulitupe, kwanza ni raini kupindukia, limajaa maji yasiyo na utama labda ule kama dawa. Halafu ukishalikata tu, tegemea kesho limeshaanza kuoza hata likiwa kwenye fridge.

3) Embe: Ohoooo, god forbid, kwa kweli naanza kuyakumbuka maembe mango, kisukari n.k. Haya ya sasa unaweza kula kama anayekula ugali, ule utamu unaoambata na ukakasi na uchungu hakuna tena, embe ni kubwa jinga, mengine utafikri unakula papai, kwa kweli ni hatari tupu

4) Mapapai: Haya ya sasa sio mapapai kabisa, mimi nakumbuka papai lilikuwa gumu, lenye utamu wa sukali, sasa mapapai yamekuwa lojolojo, papai ngozi yake ngumu ila ndani limeshameguka na kuwa lojolojo, ukimenya ngozi ngumu ila nyama ya ndani inapukutika, basi ok, liwe tamu basi, hakuna kitu ,ni kama kula makapi

Jamani, ningependa kuuliza tu, hivi Serikali haina role ya kulinda vyakula vyetu vya asili, kwa mwendo huu watoto na wajukuu wetu hawatakuja kujua the real taste ya vyakula hivi. Mimi sitaongelea kabisa kuhusu nutrition content na level ya hivi vyakula vilivyorutubishwa kwani naona mabadiliko ya ajabu ya vijana wetu kimwili, kiakili na kiafya yanaweza kuwa yamesababishwa na hivi vyakula. Je ni mamlaka gani ina kazi ya kulinda vyakula vyetu hivi kwa maslahi makubwa ya Taifa.
 
Nilidhani labda unazungumzia quality kwa maana ya export (usafirishaji wa nje ya nchi) hapo ndiyo nchi yenyewe inasema tunataka embe au ndizi za aina fulani. Lakini haya matunda ya kula inategemea na mfuko wako tu, ukitaka la auality nzuri ununue bei ghali, mfano ni embe na ndizi.
 
Sisi bado ni wazalishaji bado Yale mazao asili tunayo tumewekwa kwenye mfumo wa kibiashara kuna siku kila kitu kitakuwa kinatoka maabara hatutegemei shamba naapo ndipo tutakoboa meno tuyasage alafu ndotulie.
 
Kibiashara ina make sense. Ingawa quality ya vyakula vyetu inakuwa compromised. Ebu tujaribu kudescribe baadhi ya matunda yetu kwa sasa, kwa kuanzia tu
:
1) Nanasi: Ili la kisasa ni kubwa balaa kama mpira, ila ukilikata unakutana na maji tupu, ule utamu wa nanasi umepotea kabisa, hakuna sukali unakula kama makapi. Likikaa siku mbili limeoza. Fikilia uliponunua nanasi hili Chalinze lilikuwaje

2) Tikiti maji: Yaani ili ndilo balaa, ukiondoa rangi nyekundu iliyoboreshwa , utatamani ulitupe, kwanza ni raini kupindukia, limajaa maji yasiyo na utama labda ule kama dawa. Halafu ukishalikata tu, tegemea kesho limeshaanza kuoza hata likiwa kwenye fridge.

3) Embe: Ohoooo, god forbid, kwa kweli naanza kuyakumbuka maembe mango, kisukari n.k. Haya ya sasa unaweza kula kama anayekula ugali, ule utamu unaoambata na ukakasi na uchungu hakuna tena, embe ni kubwa jinga, mengine utafikri unakula papai, kwa kweli ni hatari tupu

4) Mapapai: Haya ya sasa sio mapapai kabisa, mimi nakumbuka papai lilikuwa gumu, lenye utamu wa sukali, sasa mapapai yamekuwa lojolojo, papai ngozi yake ngumu ila ndani limeshameguka na kuwa lojolojo, ukimenya ngozi ngumu ila nyama ya ndani inapukutika, basi ok, liwe tamu basi, hakuna kitu ,ni kama kula makapi

Jamani, ningependa kuuliza tu, hivi Serikali haina role ya kulinda vyakula vyetu vya asili, kwa mwendo huu watoto na wajukuu wetu hawatakuja kujua the real taste ya vyakula hivi. Mimi sitaongelea kabisa kuhusu nutrition content na level ya hivi vyakula vilivyorutubishwa kwani naona mabadiliko ya ajabu ya vijana wetu kimwili, kiakili na kiafya yanaweza kuwa yamesababishwa na hivi vyakula. Je ni mamlaka gani ina kazi ya kulinda vyakula vyetu hivi kwa maslahi makubwa ya Taifa.
Hata kuku, mayai, vyakula vya nafaka vimechakachuliwa, tangu lini yai likawa na viini viwili kama si chanzo cha Me kuota matiti na kuwa kisauti akidemka badala ya kuongea bass?

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Ndio serikali inawajibika kusimamia lishe ya raia wake. Isipofanya hivi inahatarisha afya zao na itasababisha kupoteza nguvu kazi kubwa sana.
 
Mimi nimeanza kufanya kilimo cha embe Bolibo ya asili ya Tabora.Wakati napata wazo hili nilishirikisha wataalamu wa kilimo na kukutana na upinzani makubwa ingawa baadaye baadhi yao walinielewa.Kifupi wengi walizingatia muda wa kuanza kuzaa kwa miembe hiyo na hii ya kisasa na wakasahau ubora na kudumu kwa miembe ya asili.Baadaye nulikutana na Mtaalam wa kilimo aliyekubaliana na wazo langu na akaniingezea faida zaidi za kulima embe Bolibo ya asili.

Kifupi serikali siyo lazima iweke sheria bali hata sisi wenyewe tunaweza kulinda mazao yetu ya asili kwa kuwa wavumilivu wa kusubiri kabla ya kuanza kuvuna,maana mfano hii embe ninayoilima inahitaji miaka saba hadi kumi ili kuanza kuzaa.Ila ikiisha anza kuzaa inadumu kwa miaka mingi sana.
 
Hata kuku, mayai, vyakula vya nafaka vimechakachuliwa, tangu lini yai likawa na viini viwili kama si chanzo cha Me kuota matiti na kuwa kisauti akidemka badala ya kuongea bass?

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
Viini viwili nadhani kuku akiwa na mafuta mengi hutaga mayai ya ajabu ajabu
 
Hata kuku, mayai, vyakula vya nafaka vimechakachuliwa, tangu lini yai likawa na viini viwili kama si chanzo cha Me kuota matiti na kuwa kisauti akidemka badala ya kuongea bass?

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
Ni kweli kabisa, tena eneo hilo ni hatari zaidi niliamua kuliacha kwanza kufocus kwenye matunda. Kwa ujumla vyakula tunavyokula kwa sasa hasa mayai, nyama za kuku , beef n.k ni lazima kuwa makini sana. Itafika sehemu nyama na mayai ambavyo ni vyakula vinavyoliwa sana vitaanza kutengenzwa mahabara kama ulaya.
 
Mimi nimeanza kufanya kilimo cha embe Bolibo ya asili ya Tabora.Wakati napata wazo hili nilishirikisha wataalamu wa kilimo na kukutana na upinzani makubwa ingawa baadaye baadhi yao walinielewa.Kifupi wengi walizingatia muda wa kuanza kuzaa kwa miembe hiyo na hii ya kisasa na wakasahau ubora na kudumu kwa miembe ya asili.Baadaye nulikutana na Mtaalam wa kilimo aliyekubaliana na wazo langu na akaniingezea faida zaidi za kulima embe Bolibo ya asili.

Kifupi serikali siyo lazima iweke sheria bali hata sisi wenyewe tunaweza kulinda mazao yetu ya asili kwa kuwa wavumilivu wa kusubiri kabla ya kuanza kuvuna,maana mfano hii embe ninayoilima inahitaji miaka saba hadi kumi ili kuanza kuzaa.Ila ikiisha anza kuzaa inadumu kwa miaka mingi sana.
Wazo zuri na tunakupongeza. Ni kweli serikali haiwezi kuingilia ila kama kutakuwepo na mkakati rasmi wa kulinda vyakula vyetu vya asili basi serikali inaweza kuhamasisha. Unajua change of social life na what majority should eat lazima iwe regulated na serikali for safety of the zitizen. Ni kupitia kwenye responsibility hii nikachombeza hoja yangu. Hongera sana kwa kulinda asili yetu.Umenikumbusha maembe ya Bolibo, ni hatari yana urojo utakimbia hasa kwa juice
 
Tupo pamoja.
 
Matunda ya asili yamepungua, embe tamu na harufu nzuri hazipo, machungwa, mananasi si yale ya zamani. Nafaka nazo mwendo ni uleule. Tunakula vyakula havina ladha na harufu nzuri kama zamani
 
Nikila wali maharage wa sasa huwa sielewi nini kimeukumba wali maharage nilioufahamu miaka ya 2000
Inasikitisha
 
Tena ule wa zamani uliowekewa nazi. Hatari yake ni asubuhi kwa kiporo, sijui kiporo cha wali maharagwe ya zamani kilikuwa vipi, ni kitamu zaidi ya fresh baada ya kupikwa. Itabidi tuanzishe mada ya kwa nini kiporo cha wali maharagwe yaliyo na nazi ni kitamu zaidi ya chakula hicho kikiwa fresh from kitchen
 
Back
Top Bottom