Braza Kede
JF-Expert Member
- Nov 1, 2012
- 3,840
- 6,844
Wakuu
Sisi wote ni mashahidi jinsi ujio wa trump ulivyoleta hekaheka nyingi kuanzia huko marekani kwenyewe, ulaya bara hindi na hata huku kwenye nchi zetu hizi weusi.
Hadi sasa hajamaliza hata miezi miwili toka aanze kazi lakini ni kama ameshakaa miaka.
Vilio vimekuwa vingi kutoka pembe zote duniani kuanzia Dar es salaam hadi Riyadh, Asmara hadi Nouakchott, kutoka Kuala Lumpur hadi visiwa vya Andaman, Johannesburg hadi Monaco, Seoul hadi Atlanta, Kathmandu hadi Sofia, Caracas hadi Tokyo. Orodha hii inaweza isiwe na mwisho.
Kifupi, karibia dunia nzima mabara yote yameathirika kwa namna fulani na ujio wa trump.
Sasa kama dunia nzima inaweza kuathiriwa kwa ukubwa kiasi hiki na ujio wa mtu mmoja tu, kwanini huyu raisi wa marekani asichaguliwe na dunia nzima tukiwemo sisi akina pangu pakavu?
Ndio, nasisi tuulizwe mnamuonaje mtu huyu? nasisi tuseme huyo 👍 au 👎.
Maana mwisho wa siku wote tunaathiriwa na maamuzi ya mtu huyu mmoja anayekaa hapo.
eti wakuu wangu au nyie mnasemaje wakuu?