Je, ni watu Gani Maarufu walioharibu fani zao au Maisha yao kwasababu Ya uzembe

Je, ni watu Gani Maarufu walioharibu fani zao au Maisha yao kwasababu Ya uzembe

maishapopote

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2009
Posts
3,408
Reaction score
6,094
Kuna watu walikua maarafu sana kwenye fani zao ila kuna matendo waliyafanya ya kizembe sana au ya kijinga mno ambayo yameharibu maisha yao au umaarufu wao, Tafadhali mtaje jina na uelezee alipobugi.

Mimi Naanza na Shkuba,
Shkuba alikua maarufu na mwenye hela nyingi mno,alishaondoka bongo na kuhamia afrika ya kusini na huku biashara zake zikienda vyema pia alishaonywa asirudi tena bongo,haikujulikana ni homesick au nn? Ila shkuba akarudi,na siku anaondoka kurudi south, alishushwa kwenye ndege maana alishaboard,mpaka leo shkuba imebaki hadithi tu yanayompata hayahadithiki,laiti kama hakujiamini sana akarudi.
 
Kwenye muziki
Mr Nice-alikuwa akipata pesa ana nunulia mikufu dubai hawekezi alifanya uzembe mpaka sasa hali mbaya.

Kwenye bongo movie
Steven Kanumba- kwa sababu ya uzembe alipoteza maisha yake, hakufa kifo cha kawaida

Kwenye soka
Mrisho Ngassa na wengine wengi tuu wangekuwa ulaya kama si blah blah zao wenyewe

Kwenye siasa
Mrema- hakuna mwanasiasa aliye wahi kuwa maarufu kama mrema hapa bongo, sku hizi amebak kituko tu.
 
WANAUME FAMILY..mapanga shaa, baada ya kujitenga kundi la Juma nature na Said fella.

WAKALI KWANZA..joslin, qjay na makamua walikuwa na nafasi nzuri ya kufanya mapinduzi ya bongofleva ndani ya Afrika mashariki.

ZANZIBAR STARS..kwenye Taarab kabla hajaondoka mzee Yusuph, Joha kassim, Mosi suleiman, zena, nk

TNG SQUARD..baada ya kutoa nyimbo safi bongo.com kundi likavunjika wakabaki wawili mwisho wakapotea mazima.

2BERRY..berry black na berry white walikuwa na nyimbo zao nzuri sana walipokuwa pamoja kama nakupenda, mimi nataka kuwa nawe

Ray C na Daz Baba wasingetumia madawa ya kulevya, tunawamiss sana kwenye game la music
 
Back
Top Bottom