Je nifanye nini ili mtoto aendelee na masomo?

sparcus

Senior Member
Joined
Feb 18, 2014
Posts
193
Reaction score
125
mimi nina mtoto wa mjomba wangu ambae yupo kidato cha pili,alikuwa anaishi na mama mkubwa baada ya wazazi wote kufariki,sasa mama mkubwa mwezi wa pili alienda shuleni kwao na kuwaambia mtoto ni mtukutu na ana tabia mbaya za udokozi amaeshindwa kuendelea kuishi nae anahitaji kumrudisha nyumbani na atamfanyia uhamisho aje kusomea singida kutoka huko dar es salaam,na kweli alimsafirisha mpaka huku,baada ya mtoto kufika singida tulimuuliza sababu hasa ikaonekana hakuna makosa makubwa ya kiasi hicho,

imebidi nimrudishe dar na kisha kumpeleka shuleni kwake lakini kuna mwalimu ambnae haitaji kumpokea na anasema kuwa alisha futwa kwakuwa mama mkubwa alisema atamfanyia uhamisho. Sasa nahitaji kufahamu ni kweli data za mwanafunzi wa form two zinaweza kufutwa ndani ya miezi miwili yakutohudhuria shuleni hata kama alishafanya mtihani wake kwakuwa tu mlezi wake alisema atamfanyia uhamisho? Na je nifanye nini ili aendelee kusoma pale shuleni na pia ni sheria gani niifate kwa ajili ya huyu mwalimu asiyehitaji kumpokea? Kwa kuwa nmefanya udadisi na baadhi ya wanafunzi wanasema ni kawaida yake kuwafukuzisha wanafunzi shule kwakuwa yeye ni mwalimu wa nidhamu,

Je nifanye nini kwa mzazi huyu anayemkatisha mtoto masomo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…