Je, nikienda sehemu ambapo hakuna Kanisa Katoliki na kuna makanisa yaliyojitenga na Kanisa Katoliki naweza kusali katika Kanisa gani?

Je, nikienda sehemu ambapo hakuna Kanisa Katoliki na kuna makanisa yaliyojitenga na Kanisa Katoliki naweza kusali katika Kanisa gani?

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Tumsifu Yesu Kristo wapendwa

Leo hii tuna vuguvugu la uekumene, kutafuta umoja ambao Yesu kabla mateso, kifo na ufufuko wake aliuombea (soma Yohane 17). Kuna mambo mengi tunayoshirikiana na makanisa mengi, na mwanzoni mwa mwaka uwa tuna juma la sala kwa ajili ya umoja wa Makanisa, kilele chake huwa Januari 25, sherehe ya Kuongoka kwa Mt. Paulo Mtume.

Tahadhari tu ni kwamba, Makanisa yaliyojitenga na Kanisa Katoliki, maana yake kuna vitu wameviacha, vingine wamevigeuka na hata kuyaongeza mengine yasiyopaswa kuwepo. Kwa kuwa hawana adhimisho la Misa, heri tu ujisalie mwenyewe. Hatari ni kwamba waweza kwenda kusali huko wakakuambukiza ukengeufu wao.
 
Kutoka chatgpt
Tumsifu Yesu Kristo!

Ikiwa uko sehemu ambapo hakuna Kanisa Katoliki, ni vyema kutambua kwamba Kanisa Katoliki linahimiza uaminifu kwa imani yake na sakramenti zake, hasa Ekaristi Takatifu ambayo ni kiini cha ibada ya Kikatoliki.

Ikiwa hakuna uwezekano wa kuhudhuria Misa, unaweza kusali binafsi, kusoma Maandiko Matakatifu, kutafakari Rozari, au kufanya Sala ya Jumapili nyumbani.

Kuhusiana na kuhudhuria ibada katika makanisa yaliyojitenga, tahadhari inahitajika. Ingawa uekumene unahimiza kuheshimu waumini wa madhehebu mengine, si kila mafundisho ya makanisa hayo yanalingana na imani Katoliki. Unashauriwa kuepuka mafundisho yanayopingana na imani Katoliki na, ikiwezekana, kusali binafsi hadi upate fursa ya kushiriki Misa Kikatoliki.

Ni vyema pia kuwasiliana na Padre au mchungaji wa Kikatoliki kwa mwongozo zaidi.

Amani ya Kristo iwe nawe! 🙏
 
Tumsifu Yesu Kristo wapendwa

Leo hii tuna vuguvugu la uekumene, kutafuta umoja ambao Yesu kabla mateso, kifo na ufufuko wake aliuombea (soma Yohane 17). Kuna mambo mengi tunayoshirikiana na makanisa mengi, na mwanzoni mwa mwaka uwa tuna juma la sala kwa ajili ya umoja wa Makanisa, kilele chake huwa Januari 25, sherehe ya Kuongoka kwa Mt. Paulo Mtume.

Tahadhari tu ni kwamba, Makanisa yaliyojitenga na Kanisa Katoliki, maana yake kuna vitu wameviacha, vingine wamevigeuka na hata kuyaongeza mengine yasiyopaswa kuwepo. Kwa kuwa hawana adhimisho la Misa, heri tu ujisalie mwenyewe. Hatari ni kwamba waweza kwenda kusali huko wakakuambukiza ukengeufu wao.
Kuna watu wàna makanisa yao kàsali huko,
Christine Shusho
Lusekelo
Mwamposa
Màsañja
Mc pilipili
 
Nimeambiwa nithibitishe uwepo wa Mungu. Ukiulizwa kama kila kitu kina mwanzo jibu ni ndio, labda kichaa aseme hapana. Sasa huo mwanzo kikomo chake ni nini? Basi kutakuwepo na mwanzo wa mwanzo. Unmoved mover as St. Thomas Aquinas put it. The problem comes when you ask such a question "who created the Unmoved mover?" No one on the earth who is able to answer it.
 
Sali Mkuu
Lutheran

Anglican

Mungu Yupo Popote Pale
 
Kama wewe ni mkatoliki endapo utaenda mahali ambapo kanisa katoliki halipo basi usiwe na shida ya kwamba utasali wapi chakufanya kwanza ulizia mahali lilipo kanisa la orthodox. kama halipo ulizia lilipo kanisa la anglican la high church. Kama halipo ulizia lilipo kanisa la anglican low church. Kama na hilo halipo basi cha kufanya ni bora tu ubaki nyumbani usali mwenyewe binafsi. angalizo! kama wewe ni mkatoliki kamwe usijichanganye kwenda kusali makanisa yafuatayo, 1 mashahidi wa jehova 2 jeshi la wokovu, pamoja na yale makanisa ambayo waumini wao husali usiku wakiwa uchi.
 
Kama unaenda kumuabudu Mungu, basi utaingia Kanisa lolote la kiroho. Ila kama ni muumuni wa dhehebu na Mapokeo ya dhehebu Bado subiri siku utakapopata Hilo Kanisa lako.
 
Back
Top Bottom