Je?nikihama kimyakimya nikosa?japo sinania ya kutapeli wala kudhulumu!

JITABOY

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2013
Posts
254
Reaction score
35
Mimi ninafanya biashara ya m pesa na jamaa yangu fulani, ktk hiyo kaz till zote za kufanyia kaz ni zangu.Tumefanya hii kaz takribani mwaka mmoja na mtendaji wa kaz ni mimi muda wote,ilitokea sikumoja nikajikuta nina loss nilmweleza mwenzangu japo baadae alinielewa tukaendelea na kaz.Lakni mimi naona sipati faida kwa hii kaz japo faida inaingia,baadae nikaambiwa na kaka yangu kwamba tukafanye kaz sehemu nyingine sasa ndo nauliza nitoke kimyakimya au?
 
Mtoto wa kiume wewe fanya maamuzi magumu usiume ume ulimi na kujiuliza simple,mwambie ukweli tu afahamu

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Kuwa muungwana ..... mrudishie shares zake ndiyo uondoke zako
 
Usijaribu kufanya hivyo katika biashara kesho na keshokutwa hauijui, kuwa muwazi mweleze kila kitu uondoke kwa amani.
 
Mweleze ukweli usimuibie hata senti, utajitia nuksi tu hukaa ufanikiwe. Wekeni mambo sawa kabla hujaondoka. Huo ndo uungwana.
 
Unataka tukushauri namna ya kumdhulumu mwenzio!
 
toa kwanza sababu ya kutaka kuondoka kimyakimya kama kweli hufanyi dhuluma!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…