Hujakosea sana, umejitahidi kwa nionavyo.
Naamini kuna swali la kuelezea elimu na uzoefu wako wa kazi ambapo hapo ndipo ungeelezea kwamba mbali na records management pia nimesoma kozi ya sales na marketing nk. Hata kwenye CV yako naamini kwamba umeweka hivyo.
Nafikiri lengo la swali hilo lilikuwa kujua ujuzi na uzoefu wako kwa mambo ya sales na marketing.
Mimi ningemjibu kwamba:
"mbali na kusomea records management pia nimesoma kozi ya sales na marketing kwa sababu ni eneo ambalo pia ninalipenda. Nina uzoefu wa kufanya shughuli za sales na marketing kwa muda wa miaka/miezi.....katika kampuni A, B/mbalimbali ambapo katika kampuni A niliweza kushirikiana na wenzangu kupandisha mauzo ya bidhaa za kampuni kufikia 60% toka 40% na pia kuongeza wateja 1,000 kwa kipindi cha miezi/miaka.... Kwa hiyo ninaamini nikipata nafasi hiyo katika kampuni yenu nitashiriki vizuri katika kuongeza mauzo na wateja "
Pia kama hauna uzoefu na kazi hiyo mfano ndiyo umemaliza chuo basi utaelezea tu kwa kina kidogo ujuzi na uelewa wako kuhusu sales na marketing na utatumia vipi huo ujuzi ulinao katika kuleta mabadiliko chanya kwenye biashara/kampuni yao.
Kwa hiyo umepatia kiasi, ilitakiwa tu uboreshe jibu zaidi ili liendane na biashara au kampuni yao yaani malengo yao, uhitaji wao nk.
Kila la kheri.