Je, nimekosea kuwapotezea baadhi ya ndugu zangu? Naomba ushauri tafadhali

Tatizo Mzee wangu hanielewi. Ila yeye nimemsamehe. Matatizo yake na marehemu mama yangu niliyaweka pembeni. Ninasimamia hali yake ya afya na matunzo ya kila siku
Umemdekeza huyo mzee sana pia
 
Maisha ya tabu uliyoyapitia ndio sababu kuu ya wewe kufanikiwa,ulifight kwa nguvu zako zote ili ufanikiwe kutokana na ubaya uliyofanyiwa,

Hapo ina maanisha kua,hao waliokufanyia ubaya nao pia wana mchango wao kwenye mafanikio yako,bila shaka kama wasingekufanyia ubaya usingepata ujasiri wa kufight na kufanikiwa,

Unaweza kuwasaidia tu haina shida ila kua nao mbali na usijenge mazowea nao,ila kama wamekuomba msamaha basi potezea tu mkuu na uwasamehe,huwezi jua kua pengine Mungu alikupitisha kwenye mtihani ule ili iwe ndio sababu ya wewe kufanikiwa leo.
 
Nimesoma reply za mleda mada ila inaonekana kabisa kua yeye tayari anayo maamuzi yake na kumshauri hapa ni kazi bure tu,sijui hata ni ushauri upi alioutaka hapa!

Au hii thd nayo ni tangazo? Kama ni tangazo basi watakuja PM.
😀😀
 
Mind your busy achana na masnitch ipo watakusnitch tena hawana jema
 
Labda niseme hv, nimesoma na kukuelewa fika ila kikubwa nachotaka kugusia mm kwenye hii historia yako ni kuhusiana na jeraha ulilonalo moyoni mwako. Kama mtu niliyekwisha pitia psychological trauma ktk makuzi yangu tena kutokea kwenye familia au niseme watu wa karibu ni ngumu kusahau hata kama ukijaaliwa kutimiza malengo yako maishani. Kuhusiana na kuwasaidia au kutowasaidia ndugu zako hapo ni bora ufuate moyo wako, najua hali unayopitia sasa inakuweka njia panda lakn fuata mwitiko wa nafsi na moyo wako, it would make you happy and no regrets. Bila kusahau kumuomba Mungu.
Mungu akubariki na familia yako
 
Achana nao hao. Watakuloga. Mchawi siku zote hawezi kukuloga mkiwa mmechukizana lazima aweke urafiki ili hata anakuharibia anakupa pole. Potezea kabisa. Ishi maisha yako waishi maisha yao. Hela hiyo nyingi sana.
 
Nakushauri Dala.... tumia lugha nzuri yenye diplomasia kwa ndg zako... kama hutaki kusaidia. tafuta sbb ya kueleweka ili waridhie.. usikatae ili mradi tu.. kuwa muungwana na mpole.
Akatae kutoa msaada kiakili ila siyo kwa uwazi. Kuwa mlifajya hivi au vile. Misaada atoe midogo midogo isiyo umiza
 
Nimesoma reply za mleda mada ila inaonekana kabisa kua yeye tayari anayo maamuzi yake na kumshauri hapa ni kazi bure tu,sijui hata ni ushauri upi alioutaka hapa!

Au hii thd nayo ni tangazo? Kama ni tangazo basi watakuja PM.
[emoji3][emoji3]

Mkuu, mimi nilijifanya kudharau kitu kinaitwa trauma mpaka nilipokuja kujitathmini baadae sana. Hawa watu walinifanya nimpuuzie hata mama yangu kabla sijajitambua.

Nakumbuka siku moja nikiwa ghetto ninatafakari uhusiano wangu na mama yangu na namna inavyomuathiri. Nililia sana usiku ule. Asubuhi nilichukua simu nikampigia mama, kuanzia siku ile, niliapa kumtetea mama yangu kwa silaha zangu zote. Hakika, mama amefariki akiwa na amani na furaha kwamba nilimtetea inavyotakiwa.

Kuhusu uamuzi inawezekana nikaonekana nimeshaamua kutokuwasaidia ila bado kuna presha na kujihoji kama nachofanya ni sahihi. Kuna mengi sijayataja kwasababu ya muda.
 
Msamehe mzee na umtunze,hao wengine ukianza tu kuwasaidia ndo wanaweza kuwa your downfall!binadamu wabaya,tena wanaweza kwenda kwa mganga wakuroge ufilisike,acha mazoea nao kabisa
Akufaaye kwa dhiki ndie rafiki,usisahau hilo
Huyo mzee naye ni wa kumchana. Kumsaheme mtu as if nothing happen hapana. Watu hawajifunzi.
 
Kaa naye umkumbushe ajue fika alifanya ujinga...

Mambo ya kusamehe as if nothing happen hapana.
 
follow your heart boss, a day will come utadrop pia, jipange ila wakazie we humans ain't good
 
Unaweza kuta hata hiyo hela wanaomba kwako wanataka kwenda kulipia gharama za kukurogea. Binadamu sio watu
 
Ishi maisha yako mkuu, binadamu ni wasahaulifu sana.
 

Ninajenga familia yangu ndo nguzo yangu
 
Halafu watu mnaenda kanisani na msikitini, hivi huwa mnaenda kwa dhumuni gani kama hamuwezi kujenga upatanishi ?
Nimejifunza hspa kua watanzanua wamejaa roho za visasi na chuki.
Ngoja niendelee kusoma maoni.
 
Halafu watu mnaenda kanisani na msikitini, hivi huwa mnaenda kwa dhumuni gani kama hamuwezi kujenga upatanishi ?
Nimejifunza hspa kua watanzanua wamejaa roho za visasi na chuki.
Ngoja niendelee kusoma maoni.

Mkuu hawa ndugu zangu niliyowataja ni walokole, kaka ni mchungaji kabisa na dada ni mlokole huwezi kuamini kama ni yeye alinifanyia vile. Hivyo hoja ya imani hapa inapoteza mashiko. Actually mimi peke yangu ndo sina ushirikiano na dini kabisa.
 
Mimi yupo jamaangu alipata matatizo nadhani wewe unasubiri mbali mno mno na ana kipato cha ukweli alisema mkuu mimi hawa nawasamehe ni umasikini tuu ndio ulikua unawasumbua kwa kuwajengea roho mbaya na mimi hii roho nisipobadilika tutakua na ukoo wenye roho mbaya aliwasaidia wote na maisha yanaenda ingawaje mpaka kesho hawaamini...hata mimi hao ningewasamehe tuu ila sio kuwa nao karibu ki vile maisha yaendelee hakuna kitu kizuri kama upo njema harafu familia ina furaha pia...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…