Je nimpe talaka au nifanyaje

Ndoa Ndoano baba, yawezekana mengi uliyafumbia macho wakati wa uchumba wenu, sasa yanakuumiza, sasa mbona hii inaoneka kama ni story ya upande mmoja tu? wewe umemfanyia nini mwenza wako labda kuna kitu na yeye hakipendi, au ulimfanyia kitu kibaya, kuwa wazi mkuu
 
Nimesoma nikahema. Yote ni kweli au umetia chumvi kidogo?? kwenye suala la haki ya ndoa hujasema, ni shwari au?

Kwa kifupi kama uliyoyasema ni kweli na kama unapenda ndoa yako isivunjike, basi tafuta ndugu wa karibu wa mkeo (mara nyingi shangazi yake wanayeelewana) halafu mweleze yote bila kuficha na umpe kazi ya kumfunda mkeo??


Umesema pia kuwa huwa anakuwa nyumbani?? Kwa hiyo ni mama wa nyumbani??? Amesoma hadi darasa la ngapi?? Maana hata House girl aliyemaliza darasa la saba anaimudu nyumba!!!

Bottom line unapoamua kuoa au kuolewa fanya kazi ya ziada kumpekua mchumba wako hadi uridhike naye angalao 75% na 25% iwe ni yale mazoea ambayo hayana madhara makubwa kwa familia mtakayoijenga. Tofauti na hapo ukisema atabadilika akiwa ndani ya nyumba unajidanganya.

Makosa ni yako, pengine hukufanya upekuzi wa kutosha wakati wa urafiki, uchumba na hatimaye kuoana. Tusaidie lipi na kuacha lipi katika hili gazeti la matatizo ulilotundika hapa. Kweli utajuta na ndiyo maana ukaona ni vema ujiite majuto hapa. Utajutaaa kuzaliwa!!!
 

Na hayo yote yasipoleta matunda, basi aoe mke wa pili mwenye kuonesha mfano na kuleta ushindani, huenda anafanya hivyo kwa kujiachia eti hana upinzani. Au mwanamke huyo hajampenda na hivyo anatafuta sababu za kufunga virago, then hakuna sababu ya kumnyima anachotaka. Kila upandacho ndicho utakachovuna. Hivyo, muonjeshe hiyo joto ya jiwe anayoitafuta. Lakini kwa hali hii, housegirl anaweza kuchukua nafasi yake bila kujua.
 
Niliona ishara mapema ila nilijua mambo yatabadilika punde akisha zoea ugenini, lakini naona muda wapita. Nimeisha ongea sana na nafanya kwa vitendo lakini ukimaliza kufanya anarudia makosa yale yale sasa nimetulia kabisa kwani naongea sana kama kasuku kwenye nyumba. Nitajaribu hii ya kanisani, kwani hata mimi nimeisi kitu kama matatizo ya akili ya kusahau. Kila siku anatafuta vitu vyake ajui alipo ziweka. Hata mtoto mdogo anajua Mama hamsikii baba si hatari hiyo!
 
Ubaya wa kungu ni mgumu kubadilisha kwani mwenzangu hapendi ndugu, nawapenda ndugu; hawapendi marafiki especially wa kike ansema hao ni wapenzi wangu akisha pata namba ya rafiki yeyote anampgia simu na kidogo kidogo naona urafiki unakufa hawaji tena nyumbani. Kwa marafiki wanaume anawafukuza kwa kuwa anapo ongea hatumii busara matokeo yake mtu akisha ongea naye kwa muda wanamwacha kama alivyo. Anapenda kufanya shopping sana, nime mwambia lazima tuangalie mbele na kuwa na akiba, anapenda kwenda out sana, nime stop hiyo kwani - pesa jamani. Anataka nikae nyumbani muda wote, nani ataleta mkate ? Kwa ufupi kwake muda ni mwingi sana kwangu sioni muda
 
...uliminya jicho moja ulipomchumbia na kumuoa, yakubidi sasa uyafunge yote mawili upate kuishi naye.

BTW, mapungufu yake yapo ndani ya uwezo wako, ...angekuwa mwasherati tungekuwa tushakuzika.
Akiwa kwao utajuaje huko mwenzangu, akija kwako we si unaona nje poa! nafikiri kucha ilifichwa sana ningelijua nisingeandika haya -
 
Majuto.... Kama walivyoshauri wadau..Mimi naona hapo mwanzo palipokuwepo neno ulikosea... ulikuwa unamfanyia kila kitu ili akukubali... akabweteka na wewe ukaona umeshinda mchezo.... Hiyo fungate baada ya kumuoa imeendelea hadi kufikia hali hii...sasa ameshindwa kurudi kwenye ukweli uu ya maisha.. UNA KAZI KUBWA MNO YA KUMREKEBISHA..TUMIA BUSARA YAKO NA FUATA MOYO WAKO KAMA KWELI UNAMPENDA..MLINDE ABAKI NDAN A NDOA NA MFUNDISHE UHALISIA WA MAISHA YA NDOA NA NYUMBA...
 
MAjuto
Aya yako ni ndefu mno ila umeongea kwa uchungu sana.
Chukua jukumu la kumfulia nguo zake na uwe unahakikisha unaporejea home anakoga na unapotoka naye hata kwenda dukani anakoga, na umnunulie wese na unyunyu wa kufaa.
Kuhusu bajeti, nunua daftari la matumizi halafu kila mnachotumia mwezi huu kiandikwe humo na gharama zake halisi utajua tu ni how much mnatumia na mtajibana vipi. Kingine kikubwa naomba umpeleke shemeji kozi yoyote ile apate ujuzi ambao utasaidia kuongeza japo tonge moja au mbili mezani.

Ukiona umemmchoka just PM me na namba yake nitampa ushauri ambao atafaidika sana
 
Duu inasikitisha sana yaani...yaani ukipata mwanamke kama huyo kwa kweli ni mipango ya mungu tu yaani na mpaka aje kubadilika ita take time kidogo.....ila kama walivyokushauri wadau hapo juu wewe usimuonee aibu mwambie hali halisi kila kitu!!
 
Nilishatengeneza Excel sheet kwenye computer na kuingiza kila column yeye ni kujaza tu risiti na jina, hilo nalo hafanyi; Nilianza na madafatari lakini madaftari yanapotea kila siku huwezi kujua yanakwenda wapi, ukija kufanya usafi unayakuta yametupwa kwenye stoo. Siwezi nikaweka kitu chochote nje nikaja nikaikuta sehemu yake. Vyombo kila mwaka lazima ninunue upya zote zinavunjwa period! Mfano sasa hivi nimegundua hatuna glasi vikombe inabisi nikanunue upya!!!
 
Pole sana, kuna jamaa alikuwa na tatizo kama lako, alipoona mke hafundishiki aliamua kumrudisha kwao kwa muda - kwa shangazi yake. Aliwaambia amempeleka mke wake afundishwe jinsi ya kutunza nyumba na familia, vinginevyo yeye atashindwa kuendelea kuishi nae - yule dada alijifunza kwa bidii maana ndoa ilikuwa hatarini!
 
Nitajaribu ushauri huu nione kama kuna mabdailiko hapo baadaye
 

Du pole sana mkuu japo mie sijafikia stage ya kuoa but kwa uliyoyasema hapo yamenistua na kunifanya nitafakari mara mbili mbili juu ya huyo mkeo....but i gues atakua na tatizo hususani la kisaikologia....jaribu kutafuta wataamu wa hilo tatizo.......maana kwa mtu mzima hawezi kua mchafu na careless kiasi hiyo....
....i hope she will change....dont give up kaka she is ua wifey......
 
Hakuna chumvi hiyo ndo summary kidogo tu ... mengine sisemi!
 
Hii kweli nilijaribu kumpa kila alichotaka naziada wakati fulani nikiwa na maana nzuri ya ubinadamu
 
........This is terrible wife!! Huyu mdada anahitaji kufundwa kwa mara ya pili.

Vile vile mtu wa kulaumiwa hapa ni mama yake kama alilelewa na mama yake mzazi. Uchafu aliokuwa nao ni kwamba kapitiliza. I'm so sorry for u, I know u love your wife ndio maana hadi leo mpo pamoja. Muhimu hapo tafuta wamama watu wazima wakae naye chini na kumueleza A to Z kuhusu mwanamke na usafi. Vp usafi wa mwili wake upoje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…