Je nimpe talaka au nifanyaje

Asee habari yako ni ndefu na imejaa kiswahili cha kizaramo asafishi,anisikii ani ani,ulichagua mwenyewe au au walikutumia kwenye mabasi ya AKIDA ukampokea,endelea kunuka swala la kumuacha liko akilini mwako mbona game hulielezei na unashiriki vipi wakati mnakulana akiwa hajaoga
 


Inategemea ulikutana naye wapi hadi mkaamua kuoana tukijua hilo ndiyo tunaweza kuanzia hapo hapo kukupa ushauri.
 
vitu vingine unaweza usiamini kabisa, hivi mwanamke utakuwaje wa hivi kweli?
 
pole majuto. wapo wanawake kama huyu wa kwako. kaka yangu alikua na kituko kama hiki, lakini alishatwangwa talaka siku nyingi. mwanamke kama huyu wa nini ndani ya nyumba sana sana atakuharibia watoto. huyu wa kaka yangu aliamua kubadilika baadae kwa sababu zake mwenyewe. jitihada ya kumrudisha kwenye tabia yake nzuri ya mwanzo zilishindikana, ikabidi apigwe talaka, ya nini kujipa ma presha watu mmekutana ukubwani.
 
vitu vingine unaweza usiamini kabisa, hivi mwanamke utakuwaje wa hivi kweli?

unaweza kukuta na yeye ni memba hapa maana jamaa kasema ananetweki masaa 24 na akatoa mchango kwa mumewe kuwa he huyu mwanamke ni waajabu sana maana nafikiri hajitambui kama yuko hivyo huo ni ugonjwana. na pia wakinamama wanaowadekeza mabintiu zao wanachangia kuwaharibu maana utakuta libinti likubwa tu liko nyumbani kwao linasubiri kuolewa lakin hapo nyumbani linapikiwa na kufuliwa na mama yake au hausgirl, wengine mpaka kuliswa nimemwona mmoja eti wazazi wake alikuwa wanamlazimisha kula akiwa na miaka 20 anashindwa wanaenda kumchemzhia maziwa na kuanza kumbembeleza anywe baada ya hapo wanamlisha chakula hapo sio mgonjwa wala nini na hakuna kazi yoyote anayofanya hapo nyumbani nguo zake zinafuliwa yeye atoke kuwatembelea marafiki zake na kurudi nyumbani sasa si ndio taipu hiyo
 
Huna tofauti na mke wangu ila wangu wangu ananipagawisha acrobatic zake usiku ndio maana hua simsemi kama wewe

na wakwangu hivyo hivyo na akrobatiki hanipi vilevile (ila heri mimi siajasema)
 
Aisee !!!hv unajifunza kutunga Hadithi za Filamu au?maana naona kama hiyo ni story tu!!!!!
 
na wakwangu hivyo hivyo na akrobatiki hanipi vilevile (ila heri mimi siajasema)
Basi kumbe kuna wanaume mna shida jamani, poleni! kweli kuta za nyumba zinaficha mengi lol. inavoelekea uko ulaya, mrudishe bongo asote mwaka hivi akijifunza uanamke na akiwa tayari arudi.
 

Pretty; huyu dada hajawahi kufundwa hata kidogo... inabidi aanze upya...

Ndugu Majuto, nakushauri kama wazazi wa huyu binti wapo, basi itisha kikao, mrudishe na uwajulishe sababu ulizoeleza hapo juu zote, then uwaambie wamfundishe na arudi kwako pale tu atakapokuwa amefuzu and yuko tayari kuhudumia familia yake.....

Kama hilo ni gumu, basi tafuta mfanyakazi. Itakupunguzia aibu
 
Majuto hii si story yako niliisikiliza Leo tena kwa kina Dina nadhani ilipostiwa kwenye Blog ya Dina Marious au wewe ndo mhusika? But ungeifupisha kidogo inatia uvivu kuisoma yote.

Pole
 
bwana majuto
ushauri wa ziondaughter na pretty ni mzuri, vile vile wengine wametoa ushauri mzuri kama kumshirikisha mama mchungaji au washauri wa ndoa wazuri kama Chriss Mauki
kwa upande wangu sahau kuhusu talaka. umeongea jambo ambalo kwangu ni zuri na linajenga ndoa nalo ni IMANI NA KUSOMA NENO LA MUNGU. inaonyesha una hofu ya Mungu, mtegemee yeye kwa sana na usichoke kusali na kuamini kuwa Mungu anaweza kukuvusha katika mtihani huo kama alivyowavusha wana wa Israel walipukuwa wanafuatiliwa na jeshi la Farao.
weka huasigeli mzuri akusaidie kazi ila sio kazi zote ( kazi ya bed rum hausgel asipewe pse)
 
Wanawake ni kiumbe cha ajabu,sometimes wanafanya mambo ya ajabu hata kama anajua ni makosa/si vizuri.Kama mwanaume hutokua makini na kukemea tabia hiyo itaendelea na siku utakapo mwambia utashangaa,anaweza kukuambia mbona siku zote nilikuwa nafanya hivyo hukuniambia.Kwakuwa tayari hali hiyo ilishajengenga,anza taratibu na kwa msimamo,usianze kwa ukali sana maana naye antakiwa kuelimishwa.NADHANI BADO HUJASHINDWA BALI HUKUWA NA MUDA MZURI KUONA UDHAIFU WAKE WAKATI ANAANZA,LAKINI SASA UNAO MUDA.TEKELEZA WAJIBU WAKO.
NAOMBA NIFAHAMISHE KAMA NDOA YENU IPO KWA MUJIBU WA DINI NA KAMA WOTE MPO DINI NA DHEHEBU MOJA KTK IMANI.
 
Majuto hii si story yako niliisikiliza Leo tena kwa kina Dina nadhani ilipostiwa kwenye Blog ya Dina Marious au wewe ndo mhusika? But ungeifupisha kidogo inatia uvivu kuisoma yote.

Pole
Samahani kuwachosha ila nilitaka niwape watu undani wa kitu chenyewe,sija soma habari hii mahala. Mzigo wangu nachekecha kutua mzigo au lah! haya ni ya kwangu tu
 
Jamani nakuhurumia sana majuto ..
1. Ulimtoa wapi?
2. Anafanya kazi?
3.mna watoto /mtoto?
Huyo anahitaji msaada hebu jaribu kumchukua hata ndugu yako wakae nae waanze kufundishana mambo ya usafi ,nini maana ya mme na kwa nini aliolewa ..
Lakini na wewe wakati wa uchumba kwani alikuwaje?
1. Alikuwa msafi na makini amekuja kubadilika sasa
navyochukia uchafu mie jamani naweza kuikimbia nyumba yako hata maji ya kunywa siombi ng'o
 
samahani kuwachosha ila nilitaka niwape watu undani wa kitu chenyewe,sija soma habari hii mahala. Mzigo wangu nachekecha kutua mzigo au lah! Haya ni ya kwangu tu

pole majuto mie nimeisoma yote naomba unijibu hayo maswali yangu kwenye ile post ..
 
pole majuto mie nimeisoma yote naomba unijibu hayo maswali yangu kwenye ile post ..
Mtoto yupo, kazi hafanyi kwa sasa ingawa ataanza Feb. Ilikuwa si rahisi kujua kama anayo uchafu kwani kuna watu kwenye nyumba, nani kasafisha hujui? Haya akija kwako kajiandaa, atajitahidi kila kitu aweke sawa, sasa yuko mwenyewe, lo! tatizo - usafi! Mie msafi sana
 
Uhitaji kupaniki ndugu yangu, hili ni tatizo dogo sana na wewe mwenyewe unaweza kulitatua. You have to make sure kuwa mkeo anapata challenges kutoka sehemu mbalimbali ndio aweze kufanya yale ambayo wewe unataka otherwise hatokuwa na mwamko na kutaka kumsukuma ndio unachemka zaidi kaka
 
Umesahau kutuambia kitu kimoja, huyu inawezekana hata pedi zilizotumika anazirundika bafuni hata wiki nzima....,Inawezekana hakufanyiwa Kitchen Party huyo,kama hili ni kweli basi jaribu kuwasiliana na ndugu zake hususani mashangazi ndio huwa wazuri sana kwa hili, waeleze huo mlolongo wa kero zako na uwaombe wakae nae chini wamfunde upya bibie na akikushinda hata baada ya lecture ya mashangazi basi vuta kitu ingine mzee mbona wako wengi tu hao..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…