Je, nina uwezo wa kupata mtoto baada ya mumewangu kuwa na korodani moja?

Makwikwi

New Member
Joined
Feb 20, 2018
Posts
2
Reaction score
2
Habari zenu wakuu.
"Mume wangu alifanyiwa upasuaji na kutolewa scrotum(Korodani) alikuwa akipata shida sana pindi anacheka utamuona anacheka mpaka machozi kumbe ndo kilio kinafwatia baada ya kicheko.

Madaktari walimfanyia upasuaji kwa kusema kwamba ingeweza kumsababishia kansa ya uzazi na sasa ana pumbu moja lakini mambo mengine yanaenda kama kawaida anasimamisha na kufanya tendo la ndoa bila tabu but uti wa mgongo unamsumbua sana tatizo hilo lilitokea tangu tupo wachumba na sasa tuna miaka mitatu hatujawahi kupata mtoto kabisa wala sijawahi kushika mimba.

Pia bao zake la kwanza ni nzito sana na nyingine anasema zinatoka kama hewa au shahawa kwa mbali sana je hataweza kupata mtoto kabisa kwasababu ya kuwa na pumbu moja naombeni mnisaidie jamani tunahangaika sana kupata mtoto kuna uwezekano wa wanaume wa aina hii kuwa na uwezo wa kumpa mwanamke mimba naomba mtusaidie jamani tunatanguliza shukrani za dhati.
 
Uwezo upo wala usijali ni tatizo la kawaida kuuzaa wanazaa vizuri sana
 
Pumbu moja inazalisha mubashara,kama unabisha nenda ukagoogle "one ballers with babies" utaona.
 
Kuwa na pumbu moja si ulemavu nendeni kwa mtaalamu wa mambo ya uzazi awapime wote kama mko sawa na awape tricks za kupata mtoto ni simpo tu dada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…