Je ninaweza kuishitaki CWT? Kwa kutotimiza wajibu wake kwangu?

mtotowatatu

Senior Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
103
Reaction score
58
Wasalaamu wakuu?. Kuna swali linanitatiza kidogo ..najiuliza kwamba mimi ni mwanachama wa CWT (CHAMA CHA WALIMU TANZANIA) na hvyo ninakatwa 2% ya mshahara wangu kila mwezi kwa ajili yao. Tatizo ni kwamba hawatimizi wajibu wao kwangu kama., kupigania maslah yangu kama mwl, kulinda hadhi yangu kama mwl na kushindwa hata kupigania mazingira bora nikiwa kazini kwangu,, naomba msaada kwa wanasheria kuna altenative ya kukishitaki chama hiki kwa kutotimiza wajibu wake kwangu?, nawasilisha

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Naona mapungufu kadhaa yapo kwako. Unaye mwakilishi hapo, matatizo hayo hayawezi kwenda mahakamani ilhali hakuna siku uliwahi omba kikao wewe bibafsi na mhusika akakugomea. Hata watumishi wanaponyima haki ni wajibu kuweka mgomo ila kuna hatua zake.
Wewe unaonekana mengine si yako bali unashinikizwa. Elewa maana ya mtumishi/mtumwa ama kasome kamsi.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Mkuu, hiyo CWT ni chama na wewe ni mwanachama wake. Ukiwa kama mwanachama hutafanikiwa kukishtaki chama chako kwa hayo madai, cha kufanya yafanyie kazi madai yako ndani ya chama chenyewe. Mfano ni harakati za kuboresha ufanisi wa utendaji wa chama au/na kubadili uongozi
 
jiendeleze kielimu kielimu mkuu; then fanya mpango wa kuachana nao hao CWT hutashinda kabsaaa mapambano. Ao CWT wana undugu na chama tawala
Umeonaaaa eeeeh

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…