Je, ninaweza kuomba kuteuliwa na Rais kuwa Mbunge?

Je, ninaweza kuomba kuteuliwa na Rais kuwa Mbunge?

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Kuna jambo ambalo ninaliwaza.

Najua kwamba Mheshimiwa Rais anazo nafasi kumi za uteuzi wa wabunge kikatiba.Najua pia kwamba anao uhuru wa kuteu mtu yeyote kwa nafasi hizo bila kuulizwa.Katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa JPM kuna mambo kadahaa ambayo nimeyaona ambayo kama angekuwa na watu sahihi yangeenda vizuri sana ila kwa sababu amezungukwa na watu ambao wakati mwingi wanamzuga anajikuta anabeba mzigo mkubwa sana katika moyo wake na akili yake

Watu hawa ndio ambao walifanya hata kwa mara ya kwanza mitandao ikazimwa wakati wa uchaguzi na hata tukaonekana kama taifa tumerudi nyuma kidemokrasia na kiusalama.Kiuhalisia kama CCM isingechukua hatua ilizochukua hali yao kisiasa ingekuwa mbaya sana ila hali ya TAIFA ingekuwa mbaya zaidi .

Sasa mimi binafsi nimejikuta nikiwaza kwa kina kwamba kuna mambo yanweza yakafanyika vizuri tu bila kuhitaji nguvu kubwa na badala yake yakahitaji akili tu kwani Kufikiri kumekuwa ni moja kati ya jamo adimu sana kipindi hiki.Kwa sababu hio basi nafikiri ni wakati sasa wa kurudishi desturi ya kufikiri kwa kina na nidhamu ya utekelezaji ila kama taifa tuepuke kurudia makosa ya miaka tano iliyopita.

Swali langu JE inawezekana kutuma maombi kwa Mh.Rais ili katika hizo nafasi chache ateue watu fulani ambao watakuwa kama timu yake ya kufikiri kwa ajili ya kupeleka taifa mbele?Wabunge 10 kama wakiteuliwa kwa umakini wanaweza kuwa chachu kubwa sana ya kupeleka mbele maendeleo ya taifa mbele.

Mimi binafsi nimewaza hivi kwa wale ambao bado wanawaza kuhusu uchaguzi uliopita nashauri turudi shambani tukalime tujipange kwa uchaguzi ujao.Wale wabunge wa upinzani ambao wamekosa nafasi basi ni wakati sasa wa wao kuwa wanaharakati na kufanya kazi karibu na wananchi ili kuhakikisha hata kama hawako katika vyombo vya maamuzi wanaendelea kuwa relevant katika siasa za nchi yetu.Kama kuna rafu zilichezwa basi wajipange kutafuta namna ya kuzishinda na kupata ushindi wa haki.

Siasa ni mchezo ambao kila mtu ana namna ya kuucheza
 
Ameshapata connection 2015-2020 hakuwa na connection tutegemee Tz kuwa kama Marekani ndani ya miaka 2
 
Awadhalilishe wapinzani, awatusi atapewa wengi wameula teuzi kwa style hio ya kumfurahisha mkuu wa meza
 
Hakuna lisilowezekana chini ya jua. Ila lazima tukubali Rais pamoja na kuwa ni kiongozi wa taasisi ya Urais; ana ubinadamu na matarajio yake kwa nani awe wapi.

Sasa je unafahamika in person ili ukiingia utaleta utofauti ambao waliopita jimboni hawana?

Na kama Rais hakujui, ni nani alie kwenye circle ya mzee akifikisha jina lako atamkubalia beyond reasonable doubt kuwa unafaa kuteuliwa ili matarajio ya Rais yatimie.

Mind you, nafasi 10 ziko aimed to serve the pleasure ya Rais; sasa mwezetu una jambo gani ambalo kwa hakika uta serve the pleasure ya Mkulu?

Kila la khere mwenzetu, umetamani jambo jema ambalo ni kati ya nafasi 10; huenda nawe ukakumbukwa na mwenye mamlaka ya uteuzi. Japo kiuhalisia sio rahisi sana.

Mwisho kuna mengi ambayo kwa sasa Watanzania tunaweza kufanya kumsaidia Rais bila kuwa wabunge; issue kubwa ni kumpata Rais.

Enzi za biblia Zakayo kwa kujua Yesu anapita alipanda juu ya mti. Leo hii kwenye enzi zetu, ukitaka sio uteuzi pekee, kama una jambo la msingi kwa maslahi ya Taifa, na Ma-RC hawana msaada au Mawaziri, ni "mti gani mrefu" wa kukwea ili kumwonda Rais Magufuli??

Kila la kheri tena, huenda uteuzi ukapata kwenye eneo ambalo mamlaka za uteuzi zitaona, "thou can serve the pleasure"

Shalom!
 
Anateua akina Jokel, kairuki, Mwari n.k wanao msifu na kusikia anacho sema, sio akina mbatia enzi za JK
 
Kama wewe ni rangi pendwa ambatanisha na picha
Ila kama wewe ni kanda pendwa ambatanisha na cheti cha kuzaliwa

Ila kama unatpkea kwa Lissu, hai na mbeya sahau hilo
 
Back
Top Bottom