Je, ninaweza kupata tena COVID19 baada ya kuugua na kupona? Na je nikipona virusi vinaondoka mwilini baada ya muda gani?

Je, ninaweza kupata tena COVID19 baada ya kuugua na kupona? Na je nikipona virusi vinaondoka mwilini baada ya muda gani?

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
JE, NIKIPONA #COVID19 NAENDELEA KUWA NA #CORONAVIRUS?

Wataalam wanasema huenda ni kwa kiasi fulani, lakini utafiti wa kundi la kwanza haujakamilika ili kuhitimisha ni kwa muda gani virusi hivyo hubaki

Utafiti wa awali kutoka Ujerumani unaashiria kuwa #COVID19 kwa kulinganishwa na SARS, mtu akipona anakuwa katika hatari ndogo ya kuambukiza virusi hivyo kwani vinakaa kwa walau siku 10 mwilini

Lakini utafiti mwingine, kufuatiwa kutibiwa kwa Madaktari wanne katika hospitali ya Wuhan, umeonesha kuwa virusi vinaweza kuendelea kuwepo mwili hadi kwa wiki mbili baada ya dalili za ugonjwa kuondoka

Baada ya dalili kuondoka, mtu akiwa hakohoi au kupiga chafya njia za kuweza kusambaza virusi hivyo inakuwa imepunguzwa sana

Ripoti nyingine iliyochaposhwa katika jarida la Kitabibu la ‘The Lancet’ ilionesha kuwa virusi hivyo vilikaa kwa muda wa siu 37 kwa mgonjwa mmoja wa China baada ya kupona


JE, NINAWEZA KUPATA TENA #COVID19 BAADA YA KUPONA?

Kupata maambukizi ya #CoronaVirus mara nyingi humaanisha huwezi kuugua tena, walau kwa muda fulani. Lakini mashaka yalianza kuonekana mwishoni mwa mwezi Februari ambapo Mwanamke mmoja mwenye miaka takriban 40 aligundulika tena na maambukizi baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali huko Osaka, Japan

Kulikuwa na hali kama hiyo katika mmoja wa Wagonjwa ndani ya meli ya Diamond Princess na pia mgonjwa mwingine kutoka Korea Kusini. Ila mashaka makubwa yalitokea kwenye tafiti iliyofanyika huko Guangdong, China ambapo asilimia 14 ya waliopona waligundulika tena kuwa na maambukizi

Hata hivyo, ni mapema sana kutoa hitimisho la kwanini watu hao walionekana kuwa tena na maambukizi. Kuna sababu nyingi zinazoweza kuleta hali hiyo ikiwemo upimaji mbaya na kuonesha mtu hana maambukizi au virusi vililala (dormant) kwa muda fulani na kuamka tena baadaye

Aidha, Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (CDC) kimesema mwitikio wa kinga ya mwili kwa ugonjwa wa #COVID19 bado haujaeleweka. “Wagonjwa wa MERS-CoV ni vigumu kupata tena maambukizi muda mfupi baada ya kuugua, ila bado haifahamiki kama hali hiyo itatokea kwa wagonjwa wa #COVID19”
 
Upvote 0
Hapo mpaka chanjo ipatikane ndio usalama utakuwepo..
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom