Je, ninayo haki ya kuongeza majina kwenye hati ya nyumba?

nyumbamungu

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2017
Posts
1,033
Reaction score
895
Katika familia yetu tupo Wanaume wa Nne na Mwanamke Mmoja, kabla Baba hajafariki aligawa mali alizokuwa nazo, (lakini hapa nazungumzia nyumba tuliokuwa tunaishi) sisi wengine tulikuwa bado wadogo.

Baada ya Baba kufariki (2001) tumegundua Marehemu Baba aliandika jina la Mjukuu (jinsia ya kike, ambaye ni mtoto wa Dada yetu naye amefariki) kwenye Hati ya Nyumba, hapo ndipo swali langu linapokuja.

Je, Sisi watoto tunayohaki kisheria ya kudai majina yetu yawepo kwenye Hati ya Nyumba?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kisheria hampaswi kuongeza jina lolote katika hati hiyo.Sababu ni kwamba kama mzee wenu aliandika jina la huyo mjukuu alifanya kwa hiari yake na bila shinikizo la mtu yeyote. Hivyo basi kwa mawanda hayo hio nyumba ni mali halali ya huyo mwenye jina katika hati hiyo na sheria inamtambua ambaye jina lake lipo katika nyaraka fulani kuwa ndiye hasa mmiliki halali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kisheria ndio mnaweza na mna ruhusiwa, nani aliteuliwa kua msamimizi wa mirathi? huyo anaweza kuibadili hati.
 
Hujamaliz

A kusoma yote mkuu. ELEWA KWANZ

Hujamalzia kusoma mkuu. Soma vizuri taarifa uwelewe vizuri kabla hujatoa Mchango wako....
 
Hatukuteua msimazi wa mirathi, je kuna muda wa kisheria kufungua shauri la msimamizi wa Mirathi?

kisheria ndio mnaweza na mna ruhusiwa, nani aliteuliwa kua msamimizi wa mirathi? huyo anaweza kuibadili hati.
 
Nyie mtakuwa na matatizo siyo bure [emoji848][emoji848]
Yani baba yenu alikataa kuwaandika watoto kama warithi akaandika mjukuu?
Yani halafu huyo mjukuu kafaje tena maskini ya Mungu?!

Mmnh ukute kuna namna!

Jamaa amewaza tu eti kichwani mwake!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaonekana baba yenu hakuwa radhi kuwarithisha nyie watoto wake hiyo nyumba.

Bila shaka alikuwa na maana yake!

Hapo kuna namna!

Halafu wengine huwa wanajiapiza mtu yeyote akifanya kinyume yamkute ya mkuta [emoji108][emoji108]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatukuteua msimazi wa mirathi, je kuna muda wa kisheria kufungua shauri la msimamizi wa Mirathi?
Ndio muda huo ni miaka mitatu tangia marehemu aondoke, ila hata kama ukichelewa una ruhusiwa kufungua upya hio mirathi ila utaje sababu iliyokuchelewesha ktk form, so bado mna muda pia.
 
Back
Top Bottom