Je, nini kinasababisha Wakulima wa Tumbaku kutofanikiwa katika maisha?

Kingfish23

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2022
Posts
490
Reaction score
485
Nipo mkoa wa Tabora kwa kipindi cha takriban miaka 10 sasa.

Nimebaini wananchi wanalima sana zao la Tumbaku kila mwaka na wanalipwa vizuri tu lakini ukiangalia mambo ya maendeleo kwa wakulima husika siyaoni zaidi ya kusubiria miradi ya Serikali kupata huduma kama afya, elimu na maji vilevile na hali yao kimaisha sio nzuri.
 
Nimeishi na kusoma Urambo kwa zaidi ya miaka 20. Muda wote huo km familia tulikuwa tunalima tumbaku. Hili zao ni la kitumwa na lina laana.

Kwanza kuna uzurumati mkubwa kutoka kwa makampuni yanayokopesha pembejeo,na makampuni yanayonunua tumbaku. Pili wizi na utapeli kwenye vyama vya msingi. Kwa hiyo unaweza kuta mkulima kalima na kuvuna vizuri lakini mwisho wa siku anakuwa na mzigo mkubwa wa madeni na makato,na tozo zisizoeleweka.

Hatimaye anapata return ndogo kabsa au asipate chochote. Kati ya wakulima 10,wawili au watatu ndo wenye ushuhuda mzuri wa mafanikio maana yake 70% to 80% ni kilio.
 
Sasa Mzee, mafanikio ya kilimo yanaendana na uzalishaji. Mkulima anauza kilo ngapi? Ambazo Thamani yake ni kiasi gani (shilingi ngapi)?

Wakulima wengi wa Tanzania wanalima kujikimu miaka nenda rudi. Hata wewe nikuulize, kwa miaka yote uliyokaa hapo mlianza na ekari ngapi na Sasa mnalima Ekari ngapi?

Kwa walio wengi utakuta ni zilezile, 1 mpaka tatu. Matumizi yameongezeka Sana mfano familia imepanuka Sana ila mapato ni yaleyale, Sasa hapo usitegemee kuona mkulima akiwa na maisha nafuu.

Siyo kosa la Ushirika.
 
Hilo zao n la kidwanzi Sana

Miaka ya 90 maeneo yasongea lilikuwa zao maarufu Sana lakn kila mwaka ilikuwa lazma usikie vifo mtu kafia katika tembe la kukaushia tumbaku kwa Moshi

Pia makampuni yakaanza upigaji hasa pembejeo kuwa ghali na vyama vya ushirika navyo kimkandamiza mkulima

Kwa sasa songea vijjn naona wameachana na zao hili wapo na Mahindi na kahawa kwa baadh ya maeneo

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Nipo mkoa wa Tabora kwa kipindi cha takriban miaka 10 sasa.

Nimebaini wananchi wanalima sana zao la Tumbaku kila mwaka na wanalipwa vizuri tu lakini ukiangalia mambo ya maendeleo kwa wakulima husika siyaoni zaidi ya kusubiria miradi ya Serikali kupata huduma kama afya, elimu na maji vilevile na hali yao kimaisha sio nzuri.
Wana nyota ya punda, just like lipumba. Fikiria usomi wake na political power aliyowah kuwa nayo na uhalisia wa nyumba yake pale Ilolangulu mizani
 
Hilo zao n la kidwanzi Sana

Miaka ya 90 maeneo yasongea lilikuwa zao maarufu Sana lakn kila mwaka ilikuwa lazma usikie vifo mtu kafia katika tembe la kukaushia tumbaku kwa Moshi

Pia makampuni yakaanza upigaji hasa pembejeo kuwa ghali na vyama vya ushirika navyo kimkandamiza mkulima

Kwa sasa songea vijjn naona wameachana na zao hili wapo na Mahindi na kahawa kwa baadh ya maeneo

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Tumbaku ya namtumbo ni ya moshi na Tabora ni ya mvukr, bei na uoenzi ni tofauti
 
Hilo zao n la kidwanzi Sana

Miaka ya 90 maeneo yasongea lilikuwa zao maarufu Sana lakn kila mwaka ilikuwa lazma usikie vifo mtu kafia katika tembe la kukaushia tumbaku kwa Moshi

Pia makampuni yakaanza upigaji hasa pembejeo kuwa ghali na vyama vya ushirika navyo kimkandamiza mkulima

Kwa sasa songea vijjn naona wameachana na zao hili wapo na Mahindi na kahawa kwa baadh ya maeneo

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Sera ya taifa ya tumbaku, taratibu na sheria zake zimebadilika, sheria za Vyama vya ushirika ndio labda kandamizi na wakulima kutolima eneo kubwa, otherwise ni uzembe ila kwa sasa tumbaku ina tija tofauti na nyuma. Grade za chini sio chini ya 0.9Usd
 
Back
Top Bottom