Je, niolewe naye? Baba yake alizaa na Mama yangu

Ndo maana nimekuja kwa ushauri maana sina jibu. Wewe ungekubali? Kwa nini?
Nimekuuliza swali wewe.. ukipata hilo jibu utafanya decision. Ila kwangu mimi nisingeweza kuolewa na A, kwani tayari namuhesabu ni ndugu yangu, mahusiano yetu yatabaki ya kaka na dada PERIOD.
 
Mmh kwangu mimi ni no! Kimaadili haiko poa..

je ukisikia kijana anetaka kukuoa baba yake na mama yako waliwahi kuwa
bofriend na girlfriend shuleni kabla hamjazaliwa?????

au waliwahi kuoana na kuachana kabla ya hamjazaliwa??????

ndo maana mwisho unauliza viongozi wa dini,wakisema sawa ni sawa tu....
 
ruksa bana, sioni blood relation hapo! Ingekuwa ni huyo dadako sawa kwako si noumer kitu
 

Mkuu inapendeza ukiwa ndani ya mada bila kutoka kwenye mstari. Huna haja ya kufanya assumption ambazo hazipo just kwa kuwa umependa kufanya hivyo.

Hoja ni kuwa Mtoto wa baba mkubwa nina muunganiko wa damu na yeye kupitia baba yangu.

Huyu Mwanaume A sina Muunganiko naye wa damu kupitia Baba wala Mama. Ila tumeunganishwa kupitia dada yangu tu. basi. Sasa mwongozo wako au ushauri uangalie kupitia hoja hii.
 
loh anaonekana au ni kweli? Usije ukaingia choo cha kiume shosti mjini hapa

Ndugu yangu tuombeane maana twajua kuwa Wanaume baba yao ni moja. Ila so far so good under close examination.
 
Ilitokea siku za nyuma bibi yangu (mdogo wa bibi) aliolewa sehemu huko kijijini, akakuta yule baba (babu) ana watoto wakubwa (sisi hatukuwahi kuwafahamu hao vijana), katika pita pita za mjini nikachumbiwa na kijana mmoja, kupeleka maelezo nyumbani wakataka kujua anatoka familia gani.. kuchunguza sana ikagundulika yule bibi yangu mdogo alishawahi kuolewa na baba wa yule kijana (bibi aliachika kitambo na hakuwahi kuzaa kwenye hiyo familia).. Ilibidi uchumba uvunjwe! maana familia ilikuja juu kuwa haiwezekani ukaolewa na mtoto wa bibi yako! upo hapo..
 
Mie naona unataka kuhalalisha jambo ambalo hata nafsi yako inakuambia si sahihi. kifupi ninyi ni ndugu na sitegemei (kaka na dada) kuoana. ila naona wewe mwenyewe unataka sisi tukuhalalishie jambo ambalo si sahihi. Nakushauri ufuate lile ambalo roho yako inataka ila maono yangu ni kuwa usiolewe na huyo kaka yako. Kama dada yako C hawezi kuolewa na huyo jamaa ni wazi kuwa hata wewe hupaswi kuolewa nae, huo ndio ukweli wa mambo, lakini kama ukilazimisha basi olewa nae tu na mchango wa harusi ntakuchangia kwani waswahili husema "UKITAKA KULA HARAM CHAGUA ILIYONONA"
Kazi ni kwako

wish you all te best in the year 2012
 

hao ndugu zako ni wajima kupita maelezo
wanahitaji maombi ya kweli......
too primitive kwa dunia ya sasa....
 


Du! Ipo kazi. Inanikumbusha habari za Bible. Kaini (muuaji wa Abeli) , Adam na Hawa. Hivi Kaini alizaa na nani na Mwanamke alikuwa ni Hawa tu mama yake?
 

Makubwa Mwaya! naona umeamua kuusemea moyo au kuniweka maneno mdomoni.
 
Why no?

Baba yake C hana undugu wowote wa damu na huyu dada.
Big lady na C wanashare mama.
Wakati anayetaka kumuona bigy lady na C wanashare baba.

Watu wanaoana mtu na binamu yake kabisa sembuse hawa?
Mmh kwangu mimi ni no! Kimaadili haiko poa..
 

kwa nini usimzalie
 
mayasa
si useme wazi hata ka ana dada wanaoana kwenu
 
Usiolewe kuna laana mnataka kutengeneza.

hakuna kitu ka laana hapa,undugu gani huo mnataka kuutengeneza kwa kuunganisha big g iliyotafunwa juzi na jana? Olewa mama kama mmependana,ongea na viongozi wako wa dini wakupigeni maombi ya kutosha muondoe iyo so called laana
 
Du! Ipo kazi. Inanikumbusha habari za Bible. Kaini (muuaji wa Abeli) , Adam na Hawa. Hivi Kaini alizaa na nani na Mwanamke alikuwa ni Hawa tu mama yake?

Duuh! Huku unakotaka kwenda sasa siko kabisa, unapotea njia. Kama ningekuwa mimi nisingeolewa kabisa maana huyo ni kaka yangu hata kama hakuna muunganiko wa damu. Naomba nitangulize samahani kwa swali hili ....hivi mama yako angekuwa hai, unadhani angekushauri vipi?
 
Halafu mtoto mtakae mzaa wewe na huyo kaka huyo mdogo wako atamuitaje huyo mwanao? Tafakari Chukua hatua

Swali zuri. Kwa kifupi hii ni INCEST. Inaweza kuwaletea madhara ya kibaiolojia kwa watoto watakaozaliwa. Kumbuka waswahili wanaosema binamu nyama ya hamu ndio wale wale wanaoamini mtoto amerogwa pale atakapozaliwa na mtindio wa ubongo au/na matatizo mengine. Mimi sikushauri uolewe nae!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…