Nkobe
JF-Expert Member
- Feb 17, 2013
- 2,204
- 3,277
Kwa wenye kujua mambo haya ya kodi wanisaidie,je kwa mfanyakazi kibarua yaani part time ambaye anatakiwa alipwe kwa lisaa mara baada ya kazi ni sawa kukatwa kodi?
ngoja nitoe maelezo kidogo.
nilipata kibarua katika ofisi moja hapa nchini yapata miaka minne sasa,kazi hii ni ya kufundisha na nikapewa barua ambayo nikama mkataba yenye kuonyesha kuwa malipo ni 15000 kwa lisaa ambapo inategemea tafundisha mara ngapi kwa juma,ila utaratibu niloukuta ni wanalipwa mwisho wa mwezi kwa kuepusha usumbufu wa kuandaa malipo kila siku,sasa imekuwa desturi wakifanya makusanyo ya malipo hayo utukata kodi,na hatuna karatasi yoyote inayoonesha kuwa tunalipwa mshahara kila mwezi,sasa zile kodi TRA zinapokelewaje?
na kinachoumiza zaidi tunaweza kuwa na madarasa mawili au matatu ambayo madai yake yanaandaliwa katika karatasi tofauti kwasababu ni level mbili tofauti zamani yalikuwa yakikatwa kodi kila karatasi linakatwa kodi kulingana na pesa iliyoko pakawa na unafuu kwetu kwani kodi inakuwa kidogo ila sasa wanaunganisa kama una madai ya madarasa manne ukakusanya ili kulipwa wana jumlisha pesa yote na kodi inakuwa kubwa unakuta mti unakatwa hata 300,000 au zaidi wakati sipewi matibabu,nauli wala NSSF je hii ni sawa?