Ndio wangeorodhesha hizo sababu za msingi na dharura zilizosababisha kuhairisha mechi watu wajue kama kwenye lile tukio kuna mchezaji wa Simba alijeruhiwa au kufa au kuna kiongozi yupi wa Simba kafa au kujeruhiwa.
Ila kwa walichokiandika wao Bado haiwezi kuipa uhalali bodi ya ligi kuhairisha mechi
1) swala la usalama limetokana na nini?
Wao wenyewe bodi ya ligi wamekiri juu kuwa Simba hawakufanya mawasiliano yeyote na maofisa wa mechi, mamlaka ya uwanja na timu mwenyeji ili waweze kuwafanyia maandalizi ya kikanuni. Hapa ni wao wenyewe Simba wamehatarisha usalama wao.
2) Kuna matukio linalopaswa kuhairisha mchezo endapo kuna kiongozi au mchezaji katika tukio hilo kajeruhiwa au kafariki lakini kuishia kusema kwamba mechi inahairishwa kwasababu tu ya uchunguzi ni kushindwa kufuata vigezo vya uhairishaji wa mechi iliyopo katika kanuni.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.