Je, nitakuwa nimekosea nikisema Wanyama pori watambuliwe kwenye katiba yetu kama watu daraja la pili?

Je, nitakuwa nimekosea nikisema Wanyama pori watambuliwe kwenye katiba yetu kama watu daraja la pili?

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Baada ya serikali ya Mh. Kikwete kwa kushirikiana na jumuia za Kimataifa kupambana na ujangili sasa nchi ina tembo wa kutosha.

Sehemu nyingi za kusini mwa Tanzania walikozingukwa na hifadhi ya Selous tembo wamekuwa wengi.

Tukichukulia mfano wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma na Wilaya ya Liwale mkoani Lindi tembo wamekuwa kero kubwa.

Mazao ya watu kila leo yanaharibiwa na tembo. Zamani serikali kupitia TAWA walikuwa wakitoa fidia kiduchu.

Yaani ilikuwa kama shamba lako limevunwa na tembo baada ya maafisa kufanya tathmini na kujiridhisha baadaye utapata mahindi ya msaada/fidia ambayo utalazimika kuchangia fedha kidogo ndipo uuziwe . Tuseme kwamba utauziwa kwa hati punguzo.

Lakini sasa baada ya zoezi la tembo kula mazao ya wananchi kuwa kubwa na kuonekana la kawaida hakuna tena fidia.

Kwa upande wa vifo

Ni mara nyingi tu wananchi wa kusini hasa hasa kutoka hizo wilaya za Tunduru na Liwale wanauwawa na tembo.

Awali fidia ya kichwa kimoja cha mtu aliyeuwawa kwa tembo ilikuwa milioni 1.

Sasa ni laki 5, sijui kuna wajanja wanapiga panga hizi rambirambi.

Turudi sasa mwananchi akimuua tembo.

Huyo mwananchi atasagwa na askari wa TAWA mpaka anyooke. Anaweza kuuwawa kabisa na akipona basi ataozea jela.

Kwa minajiri hii tembo au mnyama pori katika nchi hii ana hadhi kubwa kuliko mwananchi wa chini (mnyonge).
Yaani ukiondoa daraja la juu ambalo limebeba viongozi wa Kitaifa na familia zao daraja la pili au la kati kuna hawa wanyamapori kama tembo n.k.

Tuache unafiki, katiba iwataje hawa wanyamapori kuwa ni watu daraja la pili na maskini waganga njaa wawe daraja la tatu.
 
Back
Top Bottom