Wanapata ila inakuwa vigumu kuonekana kwa sababu yai likikomaa dume anakuwa alishanusa harufu na kulirutubisha,na hatimaye kutokumwagika.
Hapa ndipo wengi wanapofeli sasa (ikiwemo na wewe)...
Kinachomwagika (damu ya hedhi) hutoka katika kuta za mji wa mimba na wala siyo yai la uzazi!
Iko hivi... yai linapokomaa, hutumwa taarifa katika mji wa mimba na hapo kuta zile zitajiandaa kupokea yai hilo (kujiandaa kwake ni pamoja na kuvimba na kulainika kwa kuta hizo ili yai likija liweze kujishikiza vizuri)
Ikitokea yai hilo likarutubishwa na mbegu ya uzazi ya mwanaume basi yai hilo huanza safari kutoka huko kwenye mirija ya falopia kwenda kwenye mji wa mimba (uterasi) na kujishikiza na kuendelea...mpaka mtoto kuzaliwa
Lakini ikiwa hakuna urutubishaji uliofanyika basi kuta zile zitaanza kujirudisha katika hali yake ya kawaida na ndipo itatokea hali hiyo ya kutoa damu hiyo ambayo tunaita damu ya hedhi
Kuhusu yale mayai yasiyorutubishwa yanakwenda wapi hata mimi sijui lakini si kweli kwamba mayai yale ndiyo damu ya hedhi. Ingekuwa ni hivyo kwamba mayai ndo ile damu basi kwa waislamu wangechagua moja kati ya; eidha damu ya hedhi isingekuwa najisi au binadamu angekuwa najisi
Ila kwa kuangalia mechanism nyingine za kimwili wala haishangazi au kushtua kusikia mayai yale yanajipoteza ndani kwa ndani maana hata ukiangalia kujirudisha kwa zile kuta kuna maajabu kidogo
Kumradhi... turudi kwenye mada sasa
Binafsi nilisikia (fununu) kuwa nguruwe anapata hedhi lakini kwa nyani sijawahi kusikia ingawa hata kwa huyo nguruwe sidhani kama ni kweli maana mechanism ile ni mahsusi kwa binadamu tu nijuavyo!
Sent from my SM-G532F using
JamiiForums mobile app