Je, Nyerere ni kikwazo cha katiba?

Je, Nyerere ni kikwazo cha katiba?

Kadogoo

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2007
Posts
2,073
Reaction score
341
[FONT=659b3032bf4e33581116b390#240f00]Kuna kijana mmoja aliwahi kuishi katika nchi hii, na huyu kijana alikuwa anaitwa Edward Moringe Sokoine. Kijana huyu alikuwa anatoka kabila laWamasai. Sokoine aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa nchi hii na alipokuwa Waziri Mkuu alikuwa mtu wa kwanza kumrekebisha Nyerere hadharani kwakusema "Tusiseme ZidumuFikira za Mwenyekintiwa CCM, Bali TusemeZidumu Fikira Njema zaMwenyekiti wa CCM";

Ujasiri huu ulikuwa siyo wa kawaida, ilikuwa si rahisi kwa mtu yeyote kumkosoa Nyerere, Nyerere alikuwa hakosolewi, harekebishwi na wala hashauriki, alikuwa Mungu Mtu! Sokoine alipokuwa Waziri Mkuu alianzisha kampeni ya kupambana na "Wahujumu Uchumi" kwa wakati huo au kwa sasa tunawaita"Mafisadi", Sokoine aliwahi kuwapa baadhi ya vigogo wa serikali siku saba warudishe pesa za wananchi shilling millionsitini (Tsh. 60,000,000) za wakati huo ambapo dollar moja ya Kimarekani ilikuwaShillingi 20.

Vigogo hao
walidaiwa kumuuzia Lord Rajipar Meli ya serikali na pesa hazikuonekana. Basi Sokoine katika kampeni zake za kupambana na Ufisadi akawapa siku saba kwa kuwaambia kuwa anawapa Siku Saba warudishe Pesa zaWananchi, la wakishindwa atawapeleka Radio Tanzania wakawaambie Watanzania kwa Njia ya Radio PesaZao wamezipeleka Wapi?;

Mimi Naenda Dodoma Kuhutubia Bunge, Nikirudi Nipate Majibu".Kwa bahati mbaya kabla ya siku saba kutimia Sokoine alifariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea huko Dakawa – Morogoro akitokea Bungeni Dodoma.Watanzania wenzangu kama mmeyasahau haya naomba mtafute kumbukumbu kwenye maktaba za Radio Tanzaniana Magazeti ya Tanzania wakati huo (Uhuru,[/FONT][FONT=cd9800338d999ea02a1e0ac0#240f00] MWALIMU Julius Kambarage Nyerere
[/FONT]
[FONT=659b3032bf4e33582a1e0ac0#240f00]Mzalendo, Daily News &Sunday News); nakumbukayalitangazwa kwenyetaarifa ya habari wakati huo na kwenye magazeti yote yaliandika.

Sokoine alipofariki ndipo harakati za kupambana na Ufisadi za kweli zilipoishia hapo na kuzikwa rasmi nje kidogo ya mji wa Morogoro kando ya njia ya kwenda Dodoma, na baada ya hapo yakaendelea maneno yale yale ya majukwaani tu ya kulaani na kukemea rushwa na ufisadi bila yavitendo!Je, wale wakubwa wenzangu waliokula chumvi nyingi kama mimi,haya wanayakumbuka, au yakitokea haya walikuwepo Ughaibuni!? Ina maana Nyerere alikuwa hajui kwamba Kawawa ameuza meli ya Wananchi kwaShillingi million sitini? Wakati nchi ilikuwa nameli moja tu!

Sasa wale
wanao sema angekuwepo Nyerere haya yanayotokea yasingetokea, naomba waseme au wajibu hojahii.Leo hii tunashangaa ufisadi wa kawaida unaofanywa na baadhi ya mawaziri na viongozi wa umma. Sokoine alipofariki ufisadi huo wa kutisha ukaisha kimya kimya hakuna aliyejitokeza kuhoji swala hilo tena! Ndugu zangu Watanzania kabla hatujafikiri kesho kutakuwaje, lazima tukumbuke jana kulikuwa vipi. Huwezi kufanya utabiri wa hali ya uchumi (economical prognosis) wa mwaka kesho kama huna takwimu za mwaka jana.

Ukitaka kufanya utafiti wa jambo lolote lile, nilazima kwanza uelewe kitu kinachoitwa "Chanzo cha Tatizo" au kwa jina la Kiingereza "Backgroundof Problem". Bila kujua chanzo cha tatizo la Ufisadila nchi hii, hata tufanye nini au hata tumpate nani,au kitawale chama gani,hatutaweza kumaliza ufisadi.Rais Mwinyi aliukuta ufisadi, akauacha na Rais Mkapa naye akaukuta na kuendeleza yale waliofanya watangulizi wake kwa vile Katiba ni ile ile na watu niwale wale. Rais Kikwete naye hawezi kumaliza Ufisadi hata tungelala barabarani mwaka mzima,hawezi kubadilisha chochote kwa vile yeyeni mzungumzaji tu lakini System anayoisimamia ni System ile ile ya Nyerere na chama chake kile kilecha CCM. Enzi za Nyerere pamoja na Tanzania kuwa nawasomi wengi waliokuwawamefika vyuo vikuu,lakini katika uchaguzi mkuu wa Urais, Nyerere alikuwa anagombea na"Kivuli" yaani kwamba hakuna mtu mwingine mwenye sifa za kugombea nafasi ya Urais na yeye,na chini ya picha yake kulikuwa na neno "Ndiyo"na chini ya kivuli kulikuwana neno "Hapana".

Hivyo
ukichagua neno ndiyo Umemchagua Nyerere,na ukichagua neno hapana pia Umemchagua Nyerere!Huyo ndiye Nyerere niliyekuwa ninamjua mimi.Jambo la kushangaza ni kwamba katika nafasi za Ubunge walikuwepo wagombea wawili wawili wakiwakilishwa na alama ya "Jembe na Nyumba". Nakumbuka Nyerere watu walikuwa wanamtania wanamwita"Haambiliki" yaani Nyerere ni mtu aliyekuwa hapendi ushauri wa mtu yeyote yule. Wanaomjua Nyerere vizuri wanasema huwezi kumkalisha chini umshauri, hatakusikiliza,ukitaka atumie ushauri wako unatakiwa aidha uandike uache wazi aje asome bila wewe kuwepo,au uwepo chumba cha pili uongee kwa nguvu asikie lakini usijue kama anakusikiliza. Nyerere aliwahi kwenda Marekani kuomba msaada wa chakula wakati wa Rais Ronald Reagan,Rais huyo wa Marekani alimshangaa kwa nini apate shida ya kuomba chakula wakati Tanzania ni nchi yenye rutuba na mito mingi. Nyerere alida hana wataalam wazuri wa Uchumi. Reagan alimshauri kwamba ampe wakulima watano (5) wa Kimarekani waje walime chakula cha kuwatosha Watanzania wote na kingine wauze nchi za nje. Nyerere alikataa akasema yeye ni Mjamaa hataki Mabepari.
[/FONT]

[FONT=639b30389d4e33be1116b390#240f00](Makala hiii meandikwa na Dr.Noordin Jella (Ph.D. inEconomics)Former Lecturer of Mzumbe, Open & KIU – Dar, Universities.Currently: FreelanceJournalist & SeasonalPolitical AnalystEmail:norjella@yahoo.comMobile:+255 782 000 131)[/FONT]
 
Takribani miaka 28 tangu Nyerere ang'atuke uongozi wa nchi hii na miaka 13 tangu afariki dunia still mustakabali wa nchi hii unajadiliwa kwa jina la Nyerere? Hivi nchi hii wanaishi kasuku na tumbili tangu uongozi wa Mwalimu ukome? Ama la huyu Dr. Jella ni muumini mkubwa wa mizimu kiasi kwamba anaamini mzimu wa Nyerere umeikumbatia Tanzania kiganjani.
 
afadhali kwamba huyu lecturer ame retire au kuacha kuwa lecturer, kwa kweli hapa wanafunzi walikuwa hawapati mtu mzuri wa kuweza kuwafundisha, title yake na body of the matter havioani na mambo ya katiba, pili facts zake ni za kulazimisha lazimisha ili mtu uewlewe anacho taka yeye.
 
1. Corruption is and has been life in Tanzania since the days of Nyerere
2. Tanzanians have been aware of the corruption and the perpetrators who carry out all these deals
3. This corruption was well known in the U.K and a blind eye was turned to our woes (for obvious reasons)

Now my question is this to Dr.Noordin Jella , Why are we behaving as if this is a new revelation and what do we really expect the British to do apart from affirming the fact that Africans are not capable of self-governance?
 
Is this the proper pill for our problems? Kwahiyo mtoa thread anaona fahari kuendeleza ufisadi sababu ulikuwepo toka enzi zile? A group of fools!
 
Is this the proper pill for our problems? Kwahiyo mtoa thread anaona fahari kuendeleza ufisadi sababu ulikuwepo toka enzi zile? A group of fools!

Soma tena tuu utaelewa.... taratiibuu..
 
Soma tena tuu utaelewa.... taratiibuu..

Nielewe hizi mada zisizo na tija ili iweje? We are wasting our precious time in getting things that we would not get...Nyerere is dead...mkamfukue labda watu wataacha kuandamana na kufanya fujo kama yeye ndio tatizo. Mi najua tatizo ni letu wenyewe na si la mtu fulani as we would like to potray...we allowed that...
 
Back
Top Bottom