Je? Nyuki wanamaana yoyote kiroho?

Je? Nyuki wanamaana yoyote kiroho?

incredible terminator

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2016
Posts
2,498
Reaction score
4,162
Wakuu Habari ya Majukumu, leo Jioni kuna nyuki wamekuja na kutua kwenye mti ambao uko nyumban kwangu wa kivuli, hapa najiuliza namna gani naweza kuwatoa kwa usalama wa familia yangu, maana nina watoto chini ya miaka 10 wakorofi sana,

wasiwasi wangu ni Vipi endapo watawabonda mawe? Na je katika maana ya kiroho nyuki wana ishara gani wakitua katika makazi ya binadam.
 
Kwako naamini Inzi wapo, mpaka leo tuambie umepata ufunuo gani wa Kiroho kwa uwepo wa Inzi hapo kwako.
 
Wakuu Habari ya Majukumu, leo Jioni kuna nyuki wamekuja na kutua kwenye mti ambao uko nyumban kwangu wa kivuli, hapa najiuliza namna gani naweza kuwatoa kwa usalama wa familia yangu, maana nina watoto chini ya miaka 10 wakorofi sana,

wasiwasi wangu ni Vipi endapo watawabonda mawe? Na je katika maana ya kiroho nyuki wana ishara gani wakitua katika makazi ya binadam.
Inategemea, kwa sisi kwenye ukoo tangu enzi ya mababu nyuki wanakuja wanajenga kwenye boma.

Kuna baba yangu mdogo aliwafukuza kwake kuhofia watang'ata watoto.. one day wakarudi wakang'ata mtoto mmoja first born mpaka akafariki.

After there...ni biashara na mambo yake yakaanza kuyumba sana, days went by wakaja wakarudi saivi yupo sawa.

Nb. Nyumbani kwetu pia wapo, hawang'ati wala, ila kuna ndugu yetu yeye kila akija lazima wamuume😂😂😂sijui shida ni nini
 
Mizimu hiyo imechukulia nafasi hapo.

Ingawa sio nyuki wote wanakuja na dhima hii.
 
Achana na mambo ya imani mkuu.
Unachopaswa kufanya ni kuprotect you kids dhidi ya wadudu hao hatari kwa watoto watundu na wadogo kama ulivyo sema.
Ebu wawashie
moto unaofuka moshi mwingi usiku huu ili pakipambazuka wahame.
Lakini hakikisha asubuhi watu ama watoto wako hawapiti eneo hilo hadi ujiridhishe kama ni salama na nyuki walio salia wamehama.
 
Back
Top Bottom