Je, Pascal Mayalla alitudanganya alipotuaminisha hapa Jf kuwa CAG ana hadhi sawa na CJ ( Jaji Mkuu)?

Je, Pascal Mayalla alitudanganya alipotuaminisha hapa Jf kuwa CAG ana hadhi sawa na CJ ( Jaji Mkuu)?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mwanabodi Pascal Mayalla alileta uzi hapa akituelezea Uwezo wa CAG kikatiba ni sawa kabisa na Jaji Mkuu na kwamba agizo lake ni sawa na bill.

Leo Rais Magufuli amesema CAG siyo muhimili na mihimili ni mitatu tu Serikali, Bunge na Mahakama
Na kwamba CAG kwa kiswahili ni Mkaguzi na Mdhibiti mkuu wa Hesabu za serikali ILA mwenye serikali yupo.

Nakuomba mkuu Pascal Mayalla uje utolee ufafanuzi ule uzi wako vinginevyo utuombe radhi kwa kutulisha matango.

NAMSUBIRI mkuu Pascal Mayalla

Maendeleo hayana vyama!
 
Hivi Paskali hajaonja uteuzi tu, anajituma sana kuunga juhudi.... Mayala kwa kiswahili ni Njaa.
 
Siku hizi bora niamini maneno ya Pierre Konki siyo huyo mwandishi kikongwe. Amebaki na kazi ya kujikomba tu ambayo nayo haimlipi ipasavyo. Kila akichungulia karatasi ya Msigwa holaa!
 
CAG aliaminishwa na wakina Mayalla na Zitto ni zaidi ya Mihimili na akaamini hivyo. Leo hao hao wananukuu vipengele vya kukubali Rais yupo sahihi.
 
uzuri wa Paskal ni MAJI kupwa na MAJI kujaa

atajazaa quote,viambatanisho na thread zake zilizopita na sababu za mashiko

halafu atamalizia ''if u can not fight them join them"
 
Yohana mbatizaji kumbe hujamjua Paskal.

Pascal ni mtu wa kutembea juu ya akili za watu.

Kumuamini unatakiwa uhakikishe hayupo kichwani mwako.

Kwa kifupi kuwa Pascal kabadilika sana.Mbaya zaidi anaenda Mrama.

Namtabiria kabla ya january 15 mwakani atakuwa amepewa teuzi.

Natabiri pia kabla ya february mwakani Makonda atakuwa ametenguliwa.
 
Ngoja niscreenshot kabisa
 
Pascal Mayala
Ataonja Tu Unajua Vyeo Vipo
Wazigua Wanasema Tonge La Mwisho Ndiyo La Kukombea Mboga, Halafu Unaweka Na Kishimo Kwa Dole Gumba (Wazigua Wanasema Kibwinko)
Awamu Ukielekea Mwisho Atateuliwa Ale Mema
 
Mwanabodi Pascal Mayalla alileta uzi hapa akituelezea Uwezo wa CAG kikatiba ni sawa kabisa na Jaji Mkuu na kwamba agizo lake ni sawa na bill.

Leo Rais Magufuli amesema CAG siyo muhimili na mihimili ni mitatu tu Serikali, Bunge na Mahakama
Na kwamba CAG kwa kiswahili ni Mkaguzi na Mdhibiti mkuu wa Hesabu za serikali ILA mwenye serikali yupo.

Nakuomba mkuu Pascal Mayalla uje utolee ufafanuzi ule uzi wako vinginevyo utuombe radhi kwa kutulisha matango.

NAMSUBIRI mkuu Pascal Mayalla

Maendeleo hayana vyama!
Hebu shusha huo uzi tuone nani hapa anatulisha matango pori: Paskali au Yohana Mbatizaji? Uwezo wa CAG kikatiba hauwezi kuwa sawa na Jaji Mkuu, lakini wakisha chaguliwa wote hulindwa na katiba. Huwezi kuwaondoa kiurahisi kama hawakutenda kosa hata kama huwapendi.
 
Paskali wasikukatishe tamaa, nafasi za uteuzi bado zipo nyingi.
 
Back
Top Bottom