Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,817
Wakati shamra shamra za maandalizi ya uchaguzi 2017 zikiendelea kwa nguvu zote, hakuna shaka kwamba Raisi Uhuru Kenyata ataweza kushinda uchaguzi ujao, lkn swali ni kwamba Je, yule Mzee mshari Raila Odinga atakubali matokeo ya uchaguzi? Ikumbukwe kwamba yule mzee sasa hivi ana miaka nafikiri kwenye 70 hivi, hivyo kwa hali ya kawaida hii ni karata yake ya mwisho ya kujaribu kuwa Raisi wa Kenya, na hapo ndipo tatizo lilipo, sasa sijui safari hii atatumia kisingizio gani kwa maana kama Tume ya uchaguzi imeshaondolewa nafikiri, ina maana hiyo mpya ina baraka za Upinzani pia kama niko sahihi!