Je, Raila Odinga yuko ,,above the law" Kenya?

Je, Raila Odinga yuko ,,above the law" Kenya?

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,817
Ni kama vile yuko juu ya Sheria za Kenya, inaonekana kwangu Raila Odinga hawezi kukamatwa wala kushitakiwa hata afanye kosa, kwa maana Wajaluo watafanya ,,uprising" hivyo Serikali inahofia machafuko kumgusa hata kama kavunja Sheria, ...
 
Tupe mfano wa sheria aliyovunja. Kama sentensi zako zimekwisha bila ya kutoa mfano, sisi wengine hatuna cha kujibu kwasababu tutakuwa tunajibu majibu kwa kupiga ramli tu.
 
Ni kama vile yuko juu ya Sheria za Kenya, inaonekana kwangu Raila Odinga hawezi kukamatwa wala kushitakiwa hata afanye kosa, kwa maana Wajaluo watafanya ,,uprising" hivyo Serikali inahofia machafuko kumgusa hata kama kavunja Sheria, ...
Mbona umemsingle out Raila pekee, na ni sheria gani hiyo amevunja?
Wanasiasa wote wakubwa Kenya ni kama wako above the law. Hata hapo Tanzania, ni vipi yule aliyevamia studio za Clouds tv hakuchukuliwa hatua zozote?
 
Kenya machafuko kwao kawaida
Hivyo Serikali inahofia sana
 
Lkn Tanzania yetu ukiondoa Raisi wa nchi, hakuna ambaye hawezi kukamatwa, au niseme hakuna ambaye akikamatwa kutakuwa na uprising kama Kenya, leo hii Raila Odinga akishikwa patakuwa hapatoshi Kisumu, kwa kifupi hakuna Mtanzania ambaye yuko tayari kufanya fujo kwa ajili ya kumtetea Mwanasiasa!
Akihusika na kosa la jinai, bila shaka hatua za kisheria zutachukua mkondo wake. Mkono wa sheria ni ndefu na nzito kuliko hizo kelele za vyura ambayo ni vitisho vya hawa wafuasi wake.

Lakini Raila hajavunja sheria zozote, hivyo hamna sababu ya yeye kufungiwa. Hiyo itakuwa ni hujuma dhidi ya upinzani, na wafuasi wake watakuwa sawa kuandamana, na kwa kweli, dunia itamuunga mkono.
 
Ni kama vile yuko juu ya Sheria za Kenya, inaonekana kwangu Raila Odinga hawezi kukamatwa wala kushitakiwa hata afanye kosa, kwa maana Wajaluo watafanya ,,uprising" hivyo Serikali inahofia machafuko kumgusa hata kama kavunja Sheria, ...
Mheshimiwa Ndugai alimpiga mtu bakora ya kichwa hadi akazimia, vipi alifanywa nini na vyombo husika? au nae yupo juu ya sheria?
 
Hata hapo Tanzania, ni vipi yule aliyevamia studio za Clouds tv hakuchukuliwa hatua zozote?

Swali zuri sana hili halafu amejibu kisiasa hapa chini...

Barbarosa said:
Lkn Tanzania yetu ukiondoa Raisi wa nchi, hakuna ambaye hawezi kukamatwa, au niseme hakuna ambaye akikamatwa kutakuwa na uprisingkama Kenya, leo hii Raila Odinga akishikwa patakuwa hapatoshi Kisumu, kwa kifupi hakuna Mtanzania ambaye yuko tayari kufanya fujo kwa ajili ya kumtetea Mwanasiasa!
 
Back
Top Bottom