Mwalupii
Member
- Feb 9, 2013
- 28
- 14
katika siasa za tanzania tumekuwa tukiona migongano ya kimaslahi katika maamuzi mbalimbali yanayo amuliwa katika nyanja tofauti tofauti. Tumeshudia maamuzi ya bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania linapofikia maamuzi mengi yakiwa na mlengo wa chama tawala na sio utaifa, pale ambapo viongozi wa bunge hilo wanaamua kuziba masikio na kupitisha kitu chenye maslahi kwa watawala. Hata rais kikwete amekuwa mtu anaye ingilia kati pale mmbinyo wa kibajeti kutoka nje na hatmaye tunaona na kushudia kwa mara nyingine tena anakubali kwa mbinde kukutana na ukawa. Mambo ya kujiuliza atakubali kuenda kinyume na matakwa ya chama chake kuhusiana na msimamo wa chama chake kupendeza bunge liendelee,kukaa vikao vyake dodoma angali ukawa wanataka lisimame,na mambo mengine wanayo simamia kuhusiana na msimamo wao. Nauliza swari je.rais kikwete atatekeleza maadhimio yao na ukawa bila kigugumizi watakavyo adhimia na ukawa?