Je Rasimu hii ya Katiba ina Serikali 3 pekee? Hakuna mengine ya kujadili?

Je Rasimu hii ya Katiba ina Serikali 3 pekee? Hakuna mengine ya kujadili?

engmtolera

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
5,149
Reaction score
1,441
Wadau
nimejikuta naumiza kichwa kila ninaposikia matatizo ya Ardhi na mapigano kati ya wakulima na wafanyakazi yanayotokea hivi sasa Tanzania,nikajiuliza ktk hii Rasimu ya pili ya Katiba ina ongelea serikali 3 tu pekee yake?
Nikiangalia Rasimu ya pili ya katiba ktk SURA YA PILI.MALENGO MUHIMU, MISINGI YA MWELEKEO WA SHUGHULI ZA SERIKALI NA SERA ZA KITAIFA kinasema
(
v) kuweka mazingira bora kwa ajili ya kukuza kilimo, ufugaji na uvuvi kwa kuhakikisha kuwa wakulima, wafugaji na wavuvi wanakuwa na ardhi na nyenzo kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao;


ktk hiki kipengere,hakisemi wazi ni aina ipi ya ardhi itatengwa kwa ajili ya wakulima,wafugaji,ugomvi wa sasa ni kwamba wakulima wanalalamika kuwa wafugaji wanalisha mifugo yao ktk mashamba ya wakulima na tunaelewa madhara ya mifugo kama itapita kwa muda mrefu ktk ardhi ambayo inafaa kwa kilimo,kwanini wanasiasa wanaopigia kelele serikali tatu wasijikite pia ktk kutafuta dawa ya haya matatizo ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji?


Lakini pia ktk hiki kipengere kinachohusu Haki za makundi madogo katika jamii.

(c) kutengewa maeneo ya ardhi ambayo kwa desturi makundi hayo huitumia kama eneo la kuishi na kupata riziki ya chakula.

ktk hiki kipengele tunaona kuwa makundi hayo madogo ya kijamii hayajatajwa kwa majina ni makundi yapi hayo,je wakulima na wafugaji wamo ktk hilo kundi?
kiujumla rasimu hii haijataja njia mbadala itakayotumika ktk kutatua matatizo ya ardhi yanayojitokeza sasa hususani haya makundi mawili ya wakulima na wafugaji.Ni vyema wanasiasa wakaelewa kuwa serikali tatu ama mbili ama moja haitakuwa na maana kama tu mapigano ya wakulima na wafugaji hayatapatiwa ufumbuzi wa kudumu.kwani 80% ya watanzania ni wakulima na hawa hawana habari ya serikali tatu ama 2 ama 1,wao wanachokiangalia zaidi ni uwepo wa ardhi yenye rutuba itakayowasaidia wao kuweza kulima na kujipatia chakula chao cha kila siku na wafugaji pia wangependa wawe na maeneo yao rasmi yatakayowawezesha kufuga na kulisha mifugo yao pasi ya kuingilia maeneo ambayo ni mazuri kwa kilimo ama kutumia mashamba ya wakulima kama ndio maeneo ya marisho ya mifugo yao.

Kutokana na matatizo yaliyopo sasa juu ya wakulima na wafugaji ni vyema rasimu hii ikasema wazi juu ya maeneo yapi hayataruhusiwa kwa kilimo na maeneo yapi hayataruhusiwa kwa ufugaji,maeneo yapi ni kwa ajili ya wakulima na maeneo yapi ni kwa ajili ya wafugaji.
 
engmtolera Wanaenda kujadili jinsi ya kuifurahisha Zanzibar. Sijasikia mtu akizungumzia masuala mengine muhimu, wote, hata Kikwete na Waziri wake Dr Shein, wote ni serikali tatu, mbili au... basi.
 
Last edited by a moderator:
engmtolera Wanaenda kujadili jinsi ya kuifurahisha Zanzibar. Sijasikia mtu akizungumzia masuala mengine muhimu, wote, hata Kikwete na Waziri wake Dr Shein, wote ni serikali tatu, mbili au... basi.

kwa maana hiyo basi,tutegemee kupigia kura rasimu itakayokuwa imetenezwa kwa minajili ya serikali 3,2 ama 1 tu na maoni mengine ukiachana na serikali 3 hayatapata nafasi ya kujadiliwa ama kubadilishwa,hii ni hatari sana.
kwa nini hawa wananasiasa wanakimbilia zaidi ktk maswala ya kupata serikali 3,2 ama 1 na kuacha mambo mengi ya msingi ambayo ndio nguzo ya maendeleo kwa Taifa hili yakiwa hayapewi nafasi yeyote ile?
 
kwani ccm wanaogopea nini serikali tatu? mi sielewi naomba kuelimishwa wakuu.
 
Siasa imeteka nchi baba. Hatujali chochote zaidi ya siasa
 
Ndio maana nikauliza.kwani rasimu hii ya pili ya katiba inazungumzia serikali tatu peke yake?
Je hakuna mambo mengine ya msingi yanayoweza kuzungumziwa? Kwa mfano nimetaja mambo ya Ardhi na mapigano ya wakulima na wafugaji hayahitaji kupewa kipaumbele?
 
Serekali tatu!!janga la kitaifa linalokuja soon
 
Kweli kabisa.siasa imeelemea upande mmoja na tutegemee kupata katiba isiyo na mashiko makubwa na isiyotaja maslahi makubwa ya wananchi zaidi ya wanasiasa wanaotaka serikali tatu ama mbili kwa kila aina ya nguvu
 
Back
Top Bottom