Je riba ya benki kushuka?

Mudawote

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2013
Posts
10,771
Reaction score
14,129
Umofia kwenu Great Thinkers,

Je baada ya mbinyo huu wa serikali kuondoa fedha zake ma benki binafsi inaweza kupelekea haya ma benki kushindana kutafuta wateja wa kawaida.

Yaani ushindani huu unaweza kupunguza riba?

Yaani ili kuwavuta wateja ma benki haya binafsi yanaweza kupunguza riba?

Na je kwa wale wanaotarajia kuanzisha kufungua biashara ya bank inaashiria nini kwa siku zinazokuja?
 
Riba haita shuka bal wafanyakazi watapunguzwa.Tuliependa wenyewe mbwaaa .
 
Riba ndiyo kwanza zitapanda, maana hela waliyokuwa wanatukopesha serikali imeichukua, kwa hiyo wamebaki na fedha kidogo sana, na kutakuwa na screening ya kufa mtu kabla ya kukopeshwa.

Biashara nyingi zinaenda kufa this time around.
 
uchumi wa Tanzania hupo organized sana, wanaoweka fedha benki ni wachache hivyo na fedha za kwenda kukopesha watu zinakuwa ni zile kidogo zinazotokana na watu walioweka fedha kwa kuwa serikali ishachukua fedha zake
Naona Riba kushusha ni ngumu kwa kuwa watakuwa na uhaba wa fedha za kukopesha zaidi
 
itashuka kwa mikopo ya dhamana za raisilimali na kwa ile ya watumishi wa umma itapanda
 
Wacha tu na mabenk nao yamezidi riba kubwa
Nilikua na project yangu nikakopa bank ya access sh ml 90 kwa mda wa mwaka 1 na nusu rejesho lake ilikua ml 27 hapo si unaona kama ma Ni mwezi kabisa
 
kuna uwezekano riba ikaongezeka ili kuwavutia watu waweke pesa zao benki, na riba za mikopo zitaongezeka pia maana benki watafanyia biashara pesa za wateja tu ambao watalazimika kuwalipa riba kubwa kwa kadri fedha zao wanavyozikalisha muda mrefu benk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…