Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
Ubelgiji imeitolea wito nchi ya Rwanda "kusitisha msaada wowote" kwa waasi wa M23 wanaoendelea na mapigano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, baada ya uchunguzi wa Umoja wa Mataifa kubaini kuwa kundi hilo liliwaua raia 131 mwezi uliopita.
Wizara ya mambo ya nje ya Ubelgiji ilisema jana katika taarifa yake kuwa kundi la M23 lazima lisitishe mara moja uhasama na kujiondoa katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wake.
Aidha, Ubelgiji imelaani vikali mauaji ya idadi kubwa ya raia, huku ikisisitiza kuwa wahusika wa mauaji hayo hawawezi kuachwa bila kuadhibiwa.
Ubelgiji imetaka pia kukomeshwa kwa mahusiano kati ya mamlaka yoyote ya Kongo na kundi la FDLR.
Mgogoro wa M23 umesababisha kuongezeka kwa mvutano kati ya Kongo na jirani yake Rwanda, ambapo Kinshasa inaituhumu Kigali kuwaunga mkono waasi hao.
Rwanda imekana kutoa msaada wowote na kwa upande wake inaishutumu Kongo kwa kushirikiana na waasi wa FDLR wanaohusishwa na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda.