Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,119
- 4,569
Kwa zaidi ya miezi mitatu mfululizo, jiji la Mwanza limekuwa na uhaba mkubwa wa maji unao ongezaka kila kukicha. Chanzo chake cha maji ni Ziwa Victoria. Sababu zinazotolewa ni pamoja na ukame ulioikumba nchi nzima kuanzia kipindi cha kiangazi.
Ni kweli kwamba Ziwa Victoria nalo zamu hii limekauka kwa sababu ya Global Climate Change? Mbona inakuwa kama hakuna anayejali kama kule kwenye jiji la Dar ambako uhaba wa maji ulipojitokeza ndani ya wiki tatu visima virefu vinachimbwa kila sehemu?
Uhaba wa umeme unazoeleka, huu wa maji hauzoeleki.