Je, Samia ni Rais kivuli kama inavyodaiwa na vyombo vya habari vya nje?

Je, Samia ni Rais kivuli kama inavyodaiwa na vyombo vya habari vya nje?

Ashasembeko

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2017
Posts
225
Reaction score
910
Jarida la The African Intelligence liliripoti wiki iliyopita kuwa Rais mstaafu Jakaya Kikwete ndio mshauri mkuu asiye rasmi wa Rais Samia na anatumia ushawishi wake kusukuma agenda za uongozi wake zilizopigwa chini na Magufuli kama mradi wa Bagamoyo.

Jarida lengine la the Africa Report liligusia habari hii na kujaribu kuchambua kama Rais Samia ni Rais au kivuli cha Rais mstaafu Kikwete. Jaridi hili limetumia vyanzo vyao vya siri ambao vimewaeleza kuwa Kikwete amekua na ushawishi kwa Samia hususani kwenye maswala ya jumuiya ya kimataifa na Covid-19.

The Economist Intelligence Unit pia hivi karibuni liliripoti kuwa kuna watu ndani ya CCM, na baadhi ya vyombo vya usalama ndivyo vinaongoza nchi na Samia ni kama Rais mbele za watu, ila hana nguvu ya kufanya maamuzi yenye "substance".

Jana CNN walicover story ya Mbowe kupewa kesi ya Ugaidi. Mmoja wa wachambuzi (ambae alikuwa mmoja ya watu wa mwanzoni kabisa kutoa taarifa ya Magufuli kuumwa) alitabainisha mambo mawili.

1. Yaweza kuwa Samia ni kweli kabadilika na anataka kuonyesha nguvu yake kama Rais kwa kutumia mbinu za kidikteta za Magufuli.

2. Yawezekana watiifu wa serikali ya Magufuli wamegomea mabadiliko Samia anayotaka kufanya na wanapush back. Akasema Samia anaweza kuwa ameshindwa kucontrol serikali yake na viemelea vya serikali ya JPM kwenye usalama, chama na jeshi vinaendesha nchi.

Kuna baadhi ya viongozi kama Zitto Kabqe na Fatma Karume walishaanza kuona dalili za Rais kuendeshwa toka mwanzoni.

Soma hii habari


Hizi tuhuma zinafikirisha sana. Je nani anaendesha nchi? Tuna Rais kivuli? Kama ni kweli Samia anakubalije jina lake lichafuliwe? Kama ni kweli maamuzi hafanyi yy kwanini asiachie ngazi?

Tusubiri tuone tunaelekea wapi.

Sent from my SM-G975U using JamiiForums mobile app
 
Nikiwa kama SUKUMA GANG,ninasema hivii MPAMBANE NA HALI ZENU,Msoga/CDM/wanaharakati uchwara wazee wa mama anaupiga mwingi.Endeleeni na sinema zenu za kufuta legacy.

Ila tunawakumbusha tu, JPM was a president na nusu.

Kwa Sasa nchi ipo mikononi mwenu, hausiki hata chembe na sisi Sukuma gang hatuna chama,hatumsupport yeyote maana wote nyinyi kuanzia kina Gambo, Mwigulu, Dialo n.k mmeshiriki kumtusi mpaka Basi.

Ila Karma is a bitch,Ukizoea kula nyama ya mtu hutoacha na mbona mmeanza kushikiana visu mapema?
 
Wakuu wa Majeshi ya ulinzi ndo wanaongoza nchi hii hasa kwa Kumtishia maisha Mama Samia Suluhu Hassan
1.Inspector General of police(IGP)
- Simon Sirro
2.Commander of defence force(CDF)
- Venance Mabeyo
Hii ni legacy ya Magufuli
Kwanini asiwafukuze? Yeye si Amri Jeshi Mkuu au?

Sent from my SM-G975U using JamiiForums mobile app
 
Kwanini asiwafukuze? Yeye si Amri Jeshi Mkuu au?

Sent from my SM-G975U using JamiiForums mobile app
Root legacy, Hao wakuu wa Majeshi wana kila kitu, Wameshamuweka Mama Samia kwenye yao hata kwa tishio la maisha yake, Wakuu hao wa Majeshi wana mlolongo mkubwa wa watu wengi wa usalama nyuma yao na inawezekana hata ulinzi wa Raisi wenyewe ndo wanahusika kwa kulindwa na watu wao
 
nafikiri sasa hivi anajuta kosa kubwa alilofanya ni kukubali kuongozwa na kupangiwa watu wa kuwateua matokeo yake wateule wake hawamuheshimu kauli ya waziri wa fedha bungeni kumshukuru rais mstaafu kwa kumuongoza mama vizuri huku waziri wa fedha anafanya madudu na mama kushindwa kumuondoa ni ushahidi tosha yeye yuko kama picha.
 
Back
Top Bottom