Je, serikali ilitudanganya kwamba shirika la ndege ATCL linajiendesha kwa hasara?

msovero

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2019
Posts
863
Reaction score
1,534
Kuna muda nakuwa nashindwa kuielewa hii serikali yangu.

Pengine labda ni kutokana na uelewa na ufahamu mdogo nilionao kuhusu uendeshaji wa shirika letu la ndege kwani kauli na kaguzi zinazotolewa na serikali kuhusu uendeshwaji wa shirika hili zinanichanganya sana.

Kwenye ripoti ya ukaguzi wa hesabu za serikali ya mwaka 2017/2018, CAG alibainisha kuwa kuna mashirika ya serikali yanajiendesha kwa hasara na hayaingizi faida yoyote. Miongoni mwa mashirika hayo mdhibiti alitaja ni pamoja na shirika letu la ndege ATCL.

Lakini haikuishia hapo kwani katika ripoti ya CAG ya mwaka 2019/2020 makaguzi wa hesabu za serikali alienda mbali na kudai shirika letu la ndege si tu linajiendesha kwa hasara bali limeingiza hasara 'loss' ya zaidi ya billion 150 kwa miaka mitano mfululizo tangu lilipofufuliwa na hayati magufuli.

Juzi msemaji wa serikali anaibuka na kauli kwamba serikali iko mbioni kununua ndege zingine tano na tayari billion 212.95 zimeshatolewa kama malipo ya awali ya ununuzi wa ndege hizo.

Sasa hapa ndipo panapo nipa utata kwa sababu katika hali ya kawaida ni mjinga pekee ndiye anaweza kufanya biashara ambayo haiingizi faida.

Sasa Kama serikali yenyewe inakiri kwamba shirika linajiendesha kwa hasara na haliingizi faida kuna haja gani ya kwenda kununua ndege zingine wakati zilizopo tu zimeshindwa kutengeneza faida na kuliingiza taifa kwenye hasara ya mabilioni?
 
Hilo ndilo swali ulilopaswa kuuliza, habari ya kusema serikali ilidanganya haina mshiko kwenye thread yako, kwa sababu fedha inayotumika kununua ndege haitokani na faida wanayopata ATCL
 
Watu wanavuta 30% kabisa
 
Serikali itoe mchanganuo unaoonyesha wakinunua hizo ndege nyingine itachukua miaka mingapi hilo shirika lianze kupata faida?
Na ionyeshe njia zinazohitaji hizo ndege za ziada.
 
Serikali itoe mchanganuo unaoonyesha wakinunua hizo ndege nyingine itachukua miaka mingapi hilo shirika lianze kupata faida?
Na ionyeshe njia zinazohitaji hizo ndege za ziada.
ivi kwanini mchakato wa ununuzi wa hizi ndege huwa haupitii bungeni?
 
Ili Atcl ijiendeshe kwa faida nashauri watolewe wote wanaoliongoza hilo Shirika wawekwe watu wenye weledi wa kuongoza biashara kubwa kwa mafanikio , director/ ceo awekwe michael shirima ambae ni ceo wa precision air .
 
Kwenye mpira wa miguu wanaita takoling hiyo yaani kwa kiswahili unalala nae manuwari. Hujari nyekundu wala kusababisha penati cha msingi tu mashabiki waone unaupiga mwingi.
 
Sasa Kama serikali yenyewe inakiri kwamba shirika linajiendesha kwa hasara na haliingizi faida kuna haja gani ya kwenda kununua ndege zingine wakati zilizopo tu zimeshindwa kutengeneza faida na kuliingiza taifa kwenye hasara ya mabilioni?
labda ikiwa na fleet kubwa sana ya ndege ndipo itapata faida....najaribu kutafuta positivity kwenye nia ya serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…