Je Serikali imewadanganya Watumishi Vikongwe Wastaafu Kuhusu Ongezeko la Pension na Hamna Kitu?

Mkongwe Mzoefu

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2018
Posts
861
Reaction score
2,515
Mwezi Oktoba 2024 serikali kupitia Waziri Kikwete walitangaza kwa mbwembwe kubwa kuwa watumishi wote wastaafu wanaolipwa pension yao kupitia Hazina wataongezewa kiasi cha 50,000 kuanzia January 2025 baada ya kilio cha muda mrefu sana kuwa hiyo laki moja haikidhi lolote kwa wazee hao walio tumikia nchi hii katika nyanja mbalimbali ikiwemo JWTZ, Afya, Elimu, uhandisi nk kwa uaminifu mkubwa.

Kwa maumivu makubwa January hii wamegundua kuwa waziri Ridhiwani Kikwete hadi sasa awajapata hayo pasion yao ya ongezeko

Na hili ni wazi boss wao Samia Suluhu analijua sana ila naye hawajali wazee. Wazee wa Zanzibar wao muda mrefu Rais Mwinyi Alisha waongeza laki moja na kama chao cha chini cha pension ni laki mbili tokea July.

Sawa, CCM na serikali yake haimjui mwenye njaa maana wao wanajimegea keki huku wamesahau kuwa hao wazee ndio walioanza kuipika kwa uaminifu mkubwa.

Wazee hawana la kuwafanya ila waweza kuwaombea dua wanaowajali, kwa umoja wao wanaweza kuwaombea dua kina Lissu na Chadema yao wafanikiwe pengine watapata viongozi wanaojali wazee.
Hata vijana jee hamchukizwi wazazi wenu kudhalilishwa kwa kudanganywa?
 
Mkuu wameongezewa, Kuna wazee najua wamepata raise ya 50k,
Fuatilia kama ndugu yako hajaongezewa
 
Ni kweli kuwa huyu mzee nineyeguatilia kwa niaba yake hakuna mabadiliko yeyote. Labda nimtumie shujaa wa pension bungeni @Estabulaya amuulize mwigulu nchemba kunani? Au kwa vile serikali inasemekana haina hela hivyo inalipa kwa mafungu?
 
Ongezeko limelipwa kuanzia mwezi Januari, 2025. Kama mzee wako hajapata ongezeko msaidie kufuatilia PSSSF na siyo bungeni.
 
Mwezi Oktoba 2024 serikali kupitia Waziri Kikwete walitangaza kwa mbwembwe kubwa kuwa watumishi wote wastaafu wanaolipwa pension yao kupitia Hazina wataongezewa kiasi cha 50,000 kuanzia January 2025 baada ya kilio cha muda mrefu sana kuwa hiyo laki moja haikidhi lolote kwa wazee hao walio tumikia nchi hii katika nyanja mbalimbali ikiwemo JWTZ, Afya, Elimu, uhandisi nk kwa uaminifu mkubwa.

Kwa maumivu makubwa January hii wamegundua kuwa waziri Ridhiwani Kikwete hadi sasa awajapata hayo pasion yao ya ongezeko

Na hili ni wazi boss wao Samia Suluhu analijua sana ila naye hawajali wazee. Wazee wa Zanzibar wao muda mrefu Rais Mwinyi Alisha waongeza laki moja na kama chao cha chini cha pension ni laki mbili tokea July.

Sawa, CCM na serikali yake haimjui mwenye njaa maana wao wanajimegea keki huku wamesahau kuwa hao wazee ndio walioanza kuipika kwa uaminifu mkubwa.

Wazee hawana la kuwafanya ila waweza kuwaombea dua wanaowajali, kwa umoja wao wanaweza kuwaombea dua kina Lissu na Chadema yao wafanikiwe pengine watapata viongozi wanaojali wazee.
Hata vijana jee hamchukizwi wazazi wenu kudhalilishwa kwa kudanganywa?
Kikwete ni mlaghai na muongo. Hata hiyo 50k bado ni kidogo sana. Angalau ingefanywa kuwa sawa na kima cha chini cha mshahara
 
Ongezeko limelipwa kuanzia mwezi Januari, 2025. Kama mzee wako hajapata ongezeko msaidie kufuatilia PSSSF na siyo bungeni.
Ongezo lililotoka ni kwa wale wanaolipwa na PSSPF, wanaolipwa na Hazina bado bila-bila
 
Back
Top Bottom