Je, Serikali ina mpango gani wa haraka kuwatengea wananchi maeneo ya kulishia wanyama haswa wananchi wa mkoa wa Mara ? - Mhe. Agnes Marwa.
Siku ya kwanza ya Bunge la 13, tarehe 27 Januari 2026 Mhe. Agnes Marwa amesimama kidete kuihoji Serikali kuhusu hatima ya wafugaji wa Kata ya Nyantwari, Bunda, baada ya maeneo yao kutwaliwa na kuwa sehemu ya hifadhi.
Ametaka majibu ya wazi na mpango wa haraka wa kuwatengea maeneo mbadala ya ufugaji, akisisitiza kuwa wafugaji wa Mara hawawezi kuendelea kusubiri bila suluhisho la uhakika.