Je, Serikali inachukua hatua gani juu ya mishahara finyu na kandamizi inayotolewa Viwandani?

Je, Serikali inachukua hatua gani juu ya mishahara finyu na kandamizi inayotolewa Viwandani?

mills93

Member
Joined
May 26, 2016
Posts
66
Reaction score
57
Nashangaa sana Serikali inafumbia macho hili swala la mishahara viwandani, watu wana kandamizwa sana. Ujira mdogo na hawapati pesa ya maendeleo bali kula tu na nauli. Kwanni serikali imefumbia macho kuhusu hili?

Sometimes wanasema vijana hawataki kazi lakini mtu anakaa Gongo la Mboto na kazi anafanya Buguruni, anapewa elfu 5 kwa siku. Tena unakuta anafanya kazi masaa 12 kwa siku.

Jiulize anafanya maendeleo gani wakati akirudi home ana buku 2 au 3, then inabidi ale usiku na kesho aende job na anatumia nauli.


"VIJANA wake UpI!!!"
 
Huu ni unyonyaji na UKANDAMIZAJI WA HAKI ZA KIBINAADAMU.

Hakika,Hili ni la kufanyiwa KAZI.

#mfanyakazi si mtumwa
 
Hahaha nchi hii ina viwanda?! Mambo mengine ukiyasikia unaweza anza kucheka msibani.
 
Hilo ni jambo la kawaida sana kwenye mfumo wa Ubepari. Mfanyakazi wa ngazi ya chini unayefanya kazi kubwa kulipwa ujira mdogo, ili mmiliki (Bepari) apate faida kubwa na kutajirika zaidi huku wewe ukiendelea kubakia kuwa maskini.

Bahati mbaya sana hao Mabepari wana tabia ya kufungamana na Serikali ya Nchi husika, na ikibidi baadhi yao hujipenyeza na kuwa Wabunge! Hivyo inakuwa vigumu kupata mtetezi wa kuwatetea.


Nini kifanyike? Wafanyakazi wote iwe sekta binafsi au ile ya umma tunatakiwa tuungane pamoja kupitia vyama vyetu huru vya Wafanyakazi (Kwa bahati mbaya vyama vyote vya Wafanyakazi Tanzania kwa sasa vimevamiwa na kuongozwa na mamluki wa CCM) kudai stahiki zetu halali kwa Waajiri wetu kwa njia ya amani/mazungumzo mfano kudai mishahara mizuri/minono, mazingira bora ya kufanyia kazi, kupandishwa cheo/madaraja kwa wakati, nk.

Na ikishindana hiyo, basi ndipo sasa tutumie migomo, maandamano, nk.
 
Nashangaa sana serikali inafumbia macho hili swala la mishahara viwandani, watu wana kandamizwa sana. Ujira mdogo na hawapati pesa ya maendeleo bali kula tu na nauli. Kwanni serikali imefumbia macho kuhusu hili?

Sometimes wanasema vijana hawataki kazi lakini mtu anakaa Gongo la Mboto na kazi anafanya Buguruni, anapewa elfu 5 kwa siku. Tena unakuta anafanya kazi masaa 12 kwa siku.

Jiulize anafanya maendeleo gani wakati akirudi home ana buku 2 au 3, then inabidi ale usiku na kesho aende job na anatumia nauli....!!!


"VIJANA wake UpI!!!"
Hili swali ni gumu sana. Serikali ikiongeza kima cha chini sisi kama NCHI tutakuwa na gharama kubwa za uzalishaji hivyo tutakosa wawekezaji wa ndani na nje. Serikali ikiacha mishahara iliyopo itakuwa ni NCHI ya watu maskini.

Kama wewe ni mtumiajia wa bidhaa za "APPLE" ukiweza kunijibu kwanini mmiliki wa APPLE ni Wamarekani lakini UZALISHAJI wa bidhaa za "APPLE" unafanyika CHINA then utaondoa mada yako hewani
 
Back
Top Bottom