OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 426
- 685
Kama mnavyojua katika Bajeti Kuu ya Serikali ya Mwaka wa Fedha 2024/25 kuna kodi kadhaa zimependekezwa ikiwemo kodi ya kwenye Digital Assets. Bunge limeshatoa wito kwa wadau kupeleka mapendekezo yao kwenye marekebisho ya sheria ya fedha ambayo inaenda kuleta hiyo kodi ya Amali za Kidigitali.
Kwa mujibu wa muswada uliopo wa Finance Act 2024, digital Assets ni vitu vyote vyenye thamani ya fedha ikiwemo Cyptocurrency au hata tokens. Na atakayelipa kodi ya zuio ni yule mwenye platform ya kubadili assets hizo kuwa fedha halali, mathalani mwenye platform ya kubadili Cyptocurrency kuwa fedha halali.
Hata hivyo tukumbuke Crypto currency Tanzania haipo, na mtu akitaka kubadilisha anakumbana na mchakato mkubwa mara nyingi inahusisha kuondoka kidogo nchini.
Swali ni Je, Sheria hii inaenda kuruhusu Crypto currency? Na kutokana na usiri wa Cryptocurrency serikali inawezaje kuhakikisha complience kwenye hili?